Kutoka nyumbani kwa marehemu Mzee Manento ambaye alikua akiishi Kigogo Dar es salaam na taratibu za mazishi bado zinaandaliwa ingawa mpaka sasa familia bado haijapanga wapi atapumzishwa Mzee Manent0.
Godfrey David Manent0 ambaye ni mtoto wa nne wa marehemu David Manent0 kwenye interview na millardayo.com amesema ‘Mzee wetu alikua akisumbuliwa na lishe ambapo hali hii ilianza baada ya mama yetu kufariki miaka miwili iliyopita‘
‘Si kwamba alikua hapati chakula, vyakula vilikuwepo vya kutosha lakini alikua anakosa mtu wa kumpa matunzo ya ndani ya nyumba kama mke kwa hiyo tangu afariki mama mzee alikua
mpweke, matatizo ya mzee mbali na kuwa na umri mkubwa pia alikua na presha na alikua akisema mimi nina presha jamani baadae presha ikatengeneza kitu kama kisukari ikitokea presha inapanda na sukari inapanda baadae akawa anasema hadi miguu ina ganzi kidogo’
‘Mpaka mauti yanamfika tulishampeleka hospitali mara tatu, kwenye familia yetu tulikua 10 lakini 1 alifariki hivyo tumebaki 9, baba yetu alikuwa mwenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Same maeneo ya Mamba Miamba tulikuwa tunafikiria anaweza kuzikwa nyumbani kwenye asili yetu au tumzike hapahapa Dar es salaam’
‘Siku za mwisho za Mzee wetu kama alikua akikiona kifo kwa sababu siku zake za mwishomwisho alikua akisema jamani mimi naona kama sitopona alikua anao wasiwasi na kifo nadhani na ule uzee alikua akiuona na kuona siku zake zinakaribia’.
Mzee Manento amefariki akiwa na umri wa miaka 73 na kuacha watoto 9,filamu alizocheza enzi za uhai wake ni pamoja na Hero of the church,Dar To Lagos na Fake Pastor.
0 comments:
Post a Comment