Moja
kati ya majeneza yaliyohifadhiwa miili ya marehemu yakitolewa ndani ya
chumba hicho.Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa wawili hao ambao
walikuwa wakifanya kazi katika baa iitwayo Mashua iliyo ndani ya
Slipway, huku mwanamke, aliyetajwa kwa jina la Hotsan, akiwa ndiye
Meneja, walikutwa chumbani kwao wakiwa wamefariki baada ya kutoonekana
kazini tokea Jumanne, siku ambayo Watanzania walikuwa wakikumbuka miaka
15 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
WAZUNGU
wawili ambao ni mume na mke wanaodaiwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini,
wamekutwa wamekufa chumbani kwao katika nyumba waliyokuwa wakiishi
maeneo ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatano hii.
Inadaiwa
kuwa baada ya kutotokea kazini katika muda wa kawaida, wafanyakazi
wenzao walijaribu kupiga simu zao za mikononi, lakini zote zilikuwa
zikiita pasipo kupokelewa karibu mchana kutwa na hivyo kuwapa maswali
mengi yasiyo na majibu.
Siku iliyofuata, inadaiwa kuwa wafanyakazi wenzao walipojaribu tena kupiga namba hizo, simu zote mbili hazikupatikana.
0 comments:
Post a Comment