Tuesday, October 21

‘Beautiful Onyinye’ na kipenzi cha Diamond, Wema Sepetu sasa ni
mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na wasichana
wenzake penzi lake la Diamond, sasa Wema amepata kile alichokuwa
akikililia kwa muda mrefu…. Chanzo cha habari hii kutoka kwa
marafiki wa Diamond kimedai kuwa Wema amenasa ujauzito na kugundulika
hivyo walipokuwa Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na kumfanya
Diamond achanganyikiwe kwa furaha….
 Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond
kwa sasa kawa kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo
njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake…. Kugundulika
kwa ujauzito wa Wema ni baada ya kuanza kujisikia vibaya walipokuwa
Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na kizunguzungu alipokuwa hotelini
alipofikia na kulazimika kwenda hospitali kwa uchunguzi
zaidi…. Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa na
Aunt Ezekiel kwenda hospitalini waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa
sapoti Diamond na madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni cha
wiki 7… Taarifa za madaktari hao zilimfanya Wema awe kama mwehu
aliyepagawa na kurudi hotelini kwa mumewe Diamond huku akiwa na tabasamu
ambalo hapo awali Diamond hakuwahi kuliona…. Inasemekana kuwa mpaka
sasa siyo Diamond wala Wema aliyewaambia wazazi wake kuhusiana na mimba
hiyo zaidi ya watu wa karibu wa wawili hao
waliowasindikiza Afrika Kusini.
Source : blogu ya wananchi

0 comments:

-