![](http://1.bp.blogspot.com/-ON780KzHWCQ/VCOYJEyF8dI/AAAAAAAApEM/OWWEXrBGqOA/s1600/meninah.jpg)
Kikizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya
jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful
Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya
Meninah na Diamond.
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya
kwanza kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo
wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
YALE
madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la
Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya
kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo.Sexy lady wa Bongo Fleva
aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search
2012, Meninah Abdulkareem. Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na
bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili
hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo
ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi.
0 comments:
Post a Comment