Star
wa filamu nchini Jackline Wolper amesema kuwa kwasasa yupo tayari
kuolewa baada ya kupitia mambo mengi zikiwemo starehe za ujana ambazo
wengi wanaokuwa kwenye ndoa huzikimbilia na kuvunja ndoa zao kwa kuwa
hawakuzifanya kipindi wapo nje ya ndoa.
"Naamini
kabisa huu sasa ni muda muafaka kwangu, niko tayari kabisa kuwa mke
nimepitia vitu vingi ambavyo mara nyingi wengi wao huwa wanakimbilia
kwenye ndoa wakiwa bado hawajavimaliza halafu mwisho wa siku
wanazishindwa, mimi nishamaliza vyote" alisema Wolper akizungumza na
Globalpublishers pasipo kufafanua kama tayari ameshampata mchumba au la.
0 comments:
Post a Comment