Mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja ayetajwa kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini Arusha akiwa na mama yake.
USIPOSTAAJABU ya
Musa utayaona ya Firauni, ni kweli kabisa! Mtoto wa kike mwenye umri wa
mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini
hapa, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kufuatia kubakwa
na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa eneo hilo.Tukio hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama yake usiku wa manane.
Akizungumza na paparazi wetu, mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda kwenye kikundi cha akina mama.
Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu.
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke huyo.
“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema mama huyo.
Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.
Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.
Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano .
0 comments:
Post a Comment