Hii ndio shule ya msingi Kano katika kijiji cha Amani huu ni muonekano wake kwa nje.
Huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Amani Dotto Polepole akielezea changamoto mbalimbali katika shule hiyo na ukosefu wa madawati na kufanya wanafunzi kuendelea kukaa chini.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kano Shabani Masuma alisema katika kero zinazompasua kichwa ni ukosefu wa madawati na maji katika shule hiyo. |
WANAFUNZI wanaosoma katika shule ya
msingi kano iliyopo kijiji cha
Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,wanalazimika
kusoma kwa kupeana zamu kukaa kwenye madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa
na upungufu mkubwa wa madawati na kusababisha usumbufu wakati wa kuandika.
Akizungumza na waandishi wa
habari waliotembelea kijiji hicho mwalimu
mkuu wa shule hiyo Shabani Masuma alisema wanaupungufu mkubwa wa madawati ambapo
yaliyopo ni 50 tu ambapo kuanzia darasa la pili hadi la sita wanakaa chini huku
madara mawili la kwanza na la saba ndiyo wamepewa madawati hayo japo kuwa
hayatoshi.
Mwalimu Masuma alisema kutokana na
changamoto hiyo imekuwa ikisababisha wanafunzi kuwa na muandiko mbaya kwa kuwa
hakuna sehemu nzuri ya kukaa ,huku akibainisha kwamba shule hiyo ina
wanafunzi 536 kati yao wavulana ni 233
na wasichana ni 303 na kwamba darasa moja linawanafunzi zaidi ya 60.
“tunachangamoto ya
uhaba wa madawati yaliyopo ni 50 na wanafunzi
wako zaidi ya 500,wengi wao wanalazimika kukaa chini halafu wachache
darasa la kwanza na la saba ndiyo wanakalia madawati ambayo pia hugombania kwa
kuwa hayatoshi na kupeana zamu kukaa pia wastani wa wanafunzi 40 hawahudhurii
vipindi kutokana na utoro”alisema mwalimu mkuu Masuma.
Mwalimu Magesa Masolele ni
mmoja wa walimu wa shule hiyo alisema
alisema miandiko ya wanafunzi hao inakatisha tamaa hata akiandika mwanafunzi
wa darasa la tano, utafikiri ndio anaanza darasa la kwanza sababu ya kukaa
chini hakuna mpangilio mzuri wa mwandiko hivyo inawapa shida walimu hasa katika
usaishaji kwenye madaftari ndio maana wakaamuwa kupea na zamu kukalia madawati.
Naye mwenyekiti wa kijiji
hicho Doto Polepole alisema kuwa changamoto ya uhaba wa madawati ni
kubwa kwani hivi sasa serikali ya kijiji imeamua kuanza kupitisha
michango kwa wazazi, ili kuweza kuchongesha madawati wanafunzi wapate unafuu wa
kusoma na kuwaondoa kero hiyo.
Baadhi ya wazazi wa kijiji hicho
John Mlewa na Samson Masasi walisema kuwa wazazi wanatoa michango mingi ya maendeleo na kuweka wazi
kuwa suala la madawati halitafanikiwa kwa kupitia wazazi pekee kinachotakiwa ni
serikali kuingilia kati suala hilo ili kuweza kuwakomboa wanafunzi kwani
hata wao kama wazazi hawafurahishwi na hatua hiyo.
wataendelea kukaa chini mpaka
lini hata wao kama wazazi hawafurahii hali hiyo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye ni ofisa mipango Ambokisye Mwakabana alisema kuwa changamoto ya madawati ipo kwenye shule nyingi na zimetengwa fedha kwaajili ya kuchongesha madawati zaidi ya 500 na kutarajia kusambaza kwenye shule ambazo zinaupungufu mkubwa kwa kuzipatia madawati 30 kila shule ikiwa kuna shule 128 za msingi katika kata 26 za wilaya hiyo
0 comments:
Post a Comment