Na Magreth Kinabo, Dodoma
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Mpanda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA)amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni
hofu ya Mwenyezi Mungu.
Aidha
Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katikaBunge hilo, ili
kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa Katiba mpya
kwa amani na utulivu kwa kutumia kipaji chake na kuwatumikia Watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mjumbe huyo, wakati akihojiwa na
kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la
Tanzania(TBC).
Akizungumza
katika kipindi hicho, huku akinukuu kitabu cha Nabii Musa, Arfi
alisema Mwenyezi Mungu hawapendezwi na mtu mwenye jeuri na anayejivuna.
“Nimejitathimini
na kuona mimi mwenyewe ni nina nafasi gani… maaskofu, mapadre,
wachungaji na masheikh. Viongozi wetu wametusii turudi turudi napata
kiburi wapi cha kutokurudi,” alihoji Arfi.
Akirejea katika kitabu cha Qruan anasema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi na anayejivuna.
Aliongeza kuwa viongozi hao “ wana nafasi kubwa pia wanaheshima ndio maana nimeweza kurudi,””alisema.
Mjumbe
huyo alisema sasa ni wakati wa kila mtu kueleza ukweli, kwani amerejea
katika Bunge hilo, amepata bahati ya kuchangia katika sura ya nne
katika kifungu cha 43na 44 kinachohusu haki za msingi.
“Nimepata
fursa ya kutoa mapendekezo ya haki za wazee nisingewezakuwasilisha kama
ningekuwa nje. Pia haki za wafanyakazi,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu wajumbe wenzake waliosusia Bunge hilo, aliwataka kutanguliza
maslahi ya taifa.Huku akisisitiza kwamba atajitahidi kuwashawishi
wajumbe walioko nje ya Bunge hilo ili waweze kurejea.
Arfi aliwahakikishia wananchi kuwa wanawatengenezea Katiba itakayowasaidia kubadilisha ya watu wote.
0 comments:
Post a Comment