Mkuu
 wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu,Bi. Nikki Clarke akikata utepe 
kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya 
Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam,katika Jengo lao lililopo 
Mikocheni.Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh.
Mkuu
 wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia 
maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti 
wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi 
yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Kituo 
cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC,jijini Dar es 
Salaam.
Mkuu
 wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu,Bi. Nikki Clarke akibadilishana 
mawazo na aliewahi kuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Tiddo 
Mhando wakati wa hafla hiyo.
Mkuu
 wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam,Hassan Mhelela 
(kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu 
yake.
Baadhi
 ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa 
BBC waliokuwepo kwenye hafla hiyo,jijini Dar es Salaam.
Mkuu
 wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Tiddo Mhando (kulia) akiwa 
katika mazungumzo na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Ali Saleh 
pamoja na Mtangazaji Sussani Mongi.
Taswira za Studio za BBC jijini Dar.
Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar.
Wadau Salim Kikeke na Nicolas wakipitia habari kabla ya kuipeleka hewani.
BBC
 Idhaa ya Ulimwengu, imezindua ofisi zake jijini Dar es Salaam. Ofisi za
 Dar es Salaam zina studio ambazo zinatumika kuandaa matangazo maarufu 
ya redio ya asubuhi, Amka na BBC, na pia kuendesha tovuti ya 
bbcswahili.com.
Katika
 kuadhimisha uzinduzi huo, vipindi vingine viwili vya BBC Idhaa ya 
Kiswahili, Dira ya Dunia ya redio na ya TV vitaandaliwa kutoka Dar es 
Salaam katika siku hiyo ya Jumatatu Agosti 11.
Ufunguzi
 wa ofisi za Dar es Salaam ni matokeo ya mikakati ya BBC Idhaa ya 
Ulimwengu ya kuhamisha uandaaji wa vipindi vya redio na tovuti kutoka 
London kwenda Afrika Mashariki.
Ofisi
 mpya ina vifaa vya kisasa vinavyoweza kutayarisha vipindi vya redio, TV
 na huduma za habari kwa njia ya simu za mkononi. Amka na BBC, kipindi 
cha nusu saa ambacho hutangazwa Jumatatu hadi Ijumaa humulika matukio na
 taarifa zitakazojiri katika siku, sasa kitaandaliwa Dar es Salaam na 
watayarishaji na watangazaji 15.
Ofisi
 mpya pia zina watayarishaji wanaoandaa taarifa mbalimbali za kanda ya 
Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya vipindi vya TV vya Focus on Africa
 na Dira ya Dunia. Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu Nikki Clarke
 amesema:
 “Uzinduzi
 wa ofisi zetu za Dar es Salaam ni hatua kubwa katika safari yetu 
iliyoanza muda mrefu kidogo, katika kuwapa wanachotaka wasikilizaji 
katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na ambao husikiliza BBC wanapotaka
 kupata taarifa wanazoziamini na zenye uhakika. Takriban watu milioni 
12.4 – ambao ni kama nusu ya idadi ya watu wazima nchini Tanzania, 
husikiliza matangazo ya redio ya BBC kila wiki.
Na
 sasa moja ya kipindi maarufu cha BBC, Amka na BBC, kimekuja karibu 
zaidi na wasikilizaji.” Ofisi ya Dar es Salaam, ina studio mbili za 
redio ambazo zinaweza kutumika na hadi watu sita kwa wakati mmoja, na 
hivyo ni muafaka kabisa kwa kipindi kichangamfu cha Amka na BBC kwa 
ajili ya mijadala na mahojiano ya kuvutia.
Mkuu
 wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh anasema : “Ofisi mpya zinatoa 
nafasi bora kabisa kwa watayarishaji wa BBC nchini Tanzania kuimarisha 
ukusanyaji wa habari na kutoa taarifa kutoka katika eneo la Afrika 
Mashariki na Kati.
Amka
 na BBC itakuwa na uwezo mkubwa zaidi kutoa taarifa na habari 
mchanganyiko, za Afrika Mashariki na pia za dunia, pamoja na mahojiano 
ya moja kwa moja na watu mbalimbali, lakini pia makala na habari za 
kijamii.” Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa kitovu cha hatua ya BBC 
Idhaa ya Ulimwengu ya kuimarisha kuwepo kwake katika sekta ya habari 
barani Afrika.
Baada
 ya ufunguzi wa ofisi ya Nairobi mwaka 1998, BBC Idhaa ya Ulimwengu 
ilikuwa shirika la kwanza la habari la kimataifa kuwa na kituo cha 
uandaaji habari barani Afrika. Mwaka 2006 Amka na BBC ilihamishwa kutoka
 London kwenda Nairobi, na BBC Idhaa ya Ulimwengu, kwa mara nyingine 
tena ikawa shirika la kwanza la kimataifa la habari kuandaa na kutangaza
 vipindi kutoka barani Afrika. 
Katika
 hatua ya kuhamisha utayarisaji wa vipindi na taarifa za kwenye tovuti, 
kipindi maarufu cha jioni cha redio, Dira ya Dunia sasa kinatayarishwa 
Nairobi. Mwisho// Kwa taarifa zaidi wasiliana na afisa wa idara ya 
mawasiliano ya BBC Idhaa ya Ulimwengu – Lala Najafova, 
lala.najafova@bbc.co.uk.
Kwa
 wahariri: BBC Idhaa ya Ulimwengu ni shirika la utangazaji la kimataifa 
lenye idhaa nyingi za lugha mbalimbali zinazotoa huduma ya matangazo ya 
redio, TV, kwenye mtandao wa internet na pia simu za mkononi. BBC Idhaa 
ya Ulimwengu hutumia njia mbalimbali kuwafikia wasikilizaji wake wapatao
 milioni 191 duniani kote. BBC huwafikia watu milioni 265 duniani kote 
kila wiki kwa huduma zake kutoka BBC Idhaa ya Ulimwengu, BBC News TV na 
bbc.com.
 RSS Feed
 RSS Feed Twitter
 Twitter August 12, 2014
August 12, 2014
 Unknown
Unknown






























 
0 comments:
Post a Comment