Tuesday, August 12

Familia inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata ujauzito na kujifungua. 

Iko hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume alilokuwa nalo. 

Hali ilikuwa hivyo pia kwa Bianca ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa, yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa jina la Jason, lakini kutokana na kuwa na sura nzuri na umbo la kike, na hisia zake za kutaka kuishi kama mwanamke, alibadili aina ya maisha na kuishi kama mwanamke kamili. 
Wawili hao walikutana na kuamua kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa maisha ya wana ndoa, Nick akiwa baba wa familia anaevaa na kuishi kama mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi kama mwanamke kamili akiihudumia familia yake na kuvaa mavazi ya kike kama mama siku zote.
Lakini kwa mujibu wa Bianca, wawili hao wamekuwa wakishiriki tendo la ndoa kama kawaida kwa kuwa wanaamini kubadili kwao mfumo wa maisha hakuwezi kubadili viungo vyao vya mwili. Matokeo yake, baba alipata ujauzito na kujifungua. Na hivi sasa wana watoto wawili.

Cha kushangaza ni kwamba wana ndoa hao hawawachanganyi majirani tu, lakini pia wamewaficha hadi watoto wao wadogo ambao wanaamini kabisa kuwa Bianca ndiye aliyewazaa na baba yao ni Nick. Lakini siri hii itakaa hadi lini ili hali majirani wanajua na wa wanandoa hao wameshaeleza kwenye vyombo vya habari? 

 Sifahamu lini tutaanza kuwaambia ukweli, labda wakati ambapo Kai (mtoto wao mkubwa) atakapokuwa na miaka sita hivi, lakini wanatakiwa kuwa na umri mkubwa wa kutosha kuelewa. Ni muhimu wakifahamu kwa kuwa ni siri kubwa ya kuwaficha watoto wako na kama wakifahamu kupitia njia nyingine watachukia sana.
Alisema Bianca. 

Biana aliendelea kujitetea kuwa kuwa jike dume/ dume jike haielezi jinsi ulivyo. Ni kama kuwa na rangi nyeupe, nyeusi, mnene au mwembamba haielezi kitu kuhusu jinsi ulivyo. 

Kwa upande wa Nick, anasema mara ya kwanza alipopata ujauzito wa Kai alibadilika na kuishi kama mwanamke, hivyo ikawa kama yeye na mumewe wote ni wanawake. Wengi walidhani wanacheza mchezo wa kusagana. 
Lakini alipopata ujauzito wa pili ndipo alipoamua kuishi maisha yake ya kawaida kama baba na kitumbo chake. Hali ilimnyima raha mbele za watu waliokuwa wanamshangaa sana. 
 Lakini, nilipokuwa na ujauzito wa Pax (mtoto wa pili), watu walikuwa wananishangaa sana, kitu kilichonifanya nikose ujasiri. Sikuweza kuvumilia hali ile, watu kunong’onezana wakiniona, kuninyooshea video na mwisho nikawa siwezi kutoka nyumbani. Nilitoka kwenda kumuona daktari tu. Watu waliogopa kile wasichokifahamu
Alisema Nick. 

Naye Biance alipoulizwa kuhusu suala la kufanya mapenzi, hakusita kueleza wanavyoichukulia. 

 Tunaviungo vyote kwa hiyo tunavitumia. Kama tungeweza kuvibadili tungefanya hivyo, ni ingekuwa tofauti- lakini hatuwezi na watoto wanakuja kwanza.

Sasa hii tunaiitaje? Kila mmoja anatafsiri yake, kwa imani yake na uelewa wake pamoja na mila na desturi. Maajabu hayaishi!

0 comments:

-