Mbunge wa bunge la Urusi Oleg Mikheyev, ametoa pendekezo
linalowachukiza watu wengi, zaidi ikiwa ni wanawake la kuitaka serikali
kupiga marufuku uvaaji wa viatu virefu kwa wanawake.
Katika pendekezo la Mikheyev lililotumwa kwa mwenyekiti wa bodi,
ametaka kuwepo marufuku ya uvaaji viatu virefu na kuweka sheria kali ya
jinsi viatu virefu vinavyotakiwa kuwa.
Mikheyev ameandika kuwa viatu havitakiwi kuwa virefu sana kwa
wanawake kwa kuwa na urefu wa nchi mbili mpaka nne kufikia urefu wa nchi
sita si kitu bora sana, hatua iliyoungwa mkono na baadhi ya wabunge.
0 comments:
Post a Comment