Ofisi
ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG imeamplfy kwamba kitendo cha
Serikali kukosa nyaraka za mali zake kumechangia baadhi ya watendaji
wasio waaminifu kutumia mwanya huo kujisogezea mali za umma.
Katika ripoti yake ya Ukaguzi kwa mwaka 2013 CAG Ludovick Utouh
amesema ofisi yake imebaini upotevu wa magari 11 yaliyonunuliwa kwa
ajili ya matumizi na mamlaka ya maendeleo na biashara Tanzania
(TanTrade) ambayo hadi sasa hayafahamiki yalipo.
Ofisi yake inalifanyia uchunguzi suala hilo na tayari imegundua hayo
magari yalisajiliwa kwa namba binafsi badala ya namba za serikali huku
akisema ‘wizara ya viwanda na biashara ilinunua magari kwa ajili ya bodi
ya biashara na tunaomba kusema magari hayo tumejaribu kuyafatilia
lakini hayaonekani na hayajulikani yalipo na ni magari mapya
yalinunuliwa kwa ajili ya TanTrade
lakini TanTrade wenyewe wanasema
hawajayapokea na Wizara inasema haijui yako wapi’
Kwenye
sentensi nyingine kamati ya kudumu ya bunge serikali za mitaa LAAC
imesikitishwa na kitendo cha halmashauri ya jiji la Mwanza kupata hati
chafu za hesabu kwa mwaka 2013 na kupanga kwenda kufanya uchunguzi juu
ya kilichochangia kutokea kwa hiyo ishu.
Mwenyekiti wa LAAC Rajabu Mbaruku amesema kamati yake imepata
upinzani ilipotaka kukagua hesabu za halmashauri hiyo baada ya watendaji
wake kukimbia ofisi zao kwa hiyo kamati ikashindwa kufanya mahojiano na
ukaguzi katika jiji la Mwanza.
‘Sasa tutakapoanza shughuli zetu mkoa wa kwanza utakua Mwanza
Spika wa Bunge ametangaza kupanga ratiba ili kutoa fursa kwa ripoti
hiyo ya hesabu za serikali kwa mwaka ulioshia June 30 2013 kujadiliwa na
wabunge.
0 comments:
Post a Comment