Huyu
mrembo anaitwa V Stiviano ambae ndio alivujisha maongezi ya simu kati
yake na bilionea Donald Sterling ambae alitoa maneno mazito yenye
ubaguzi dhidi ya watu weusi kwa kusema hataki kuwaona watu hao
wakihudhuria kwenye mechi za timu ya basketball anayoimiliki iitwayo L.A
Clippers.
Toka hii ishu imevuja Stiviano ambae alikua ni ‘nyumba ndogo’ ya
Donald amekua akikwepa waandishi wa habari ambapo aliamua kuvaa kifaa
maalum kabisa ili kuepuka kuhojiwa na waandishi wa habari.
Mmoja kati ya Wamarekani waliotoa maoni yao kuhusu Stiviano alisema
‘huyu binti anaweza kuwa mpuuzi wa kupindukia… japokua mimi ni Mweusi,
sijali kama Donald alikua mbaguzi ama la… msichana kama huyu anawezaje
kumsaliti mtu aliempa magari ya kifahari Ferarri, Bentley mbili na
nyumba ya kifahari? huyu binti hajatenda haki’
Bilionea wa kimarekani Donald Sterling alikiri kwamba
sauti
iliyosikika ikitoa maneno ya kibaguzi ni yake hivyo akaadhibiwa kwa
kutojihusisha na timu yake milele na kulazimishwa kuiuza timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment