Tuesday, May 27

malaria
Damu kutoka kwenye kundi moja la watoto wa kitanzania iliyogundulika kuwa na kinga ya asili dhidi ya Malaria, sasa inawasaidia wanasayansi hao kutoka nchini Uingereza  kutengeneza chanjo madhubuti ya ugonjwa huo.hatari duniani.
Wanasayansi hao walikusanya sampo za kawaida za damu kwa watoto 1000 kutoka nchini Tanzania na kugundua kuwa damu ya takribani watoto sita kati ya 100 ina uwezo wa kupambana na vimelea vya Malaria.
malaria2
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha tiba cha Brown wamegundua kuwa
miili ya watoto hawa inatengeneza chembechembe hai zinazopambana na vimelea vinavyosababisha Malaria.
Majaribio yamefanyika kwa kutumia panya na kugundulika kuwa iliwakinga kutopata ugonjwa huo hatari ambapo wanasayansi wanasema kukamilika kwa utafiti wake kutasaidia kutengeneza chanzo bora itakayopambana na vimelea vinavyosababisha Malaria katika mwili wa binadamu.

0 comments:

-