Hatimaye serikali ya Malaysia imeachia hadharani data halisi
zilizotumika kugundua kuwa ndege iliyopotea ya MH370 ilianguka Kusini
mwa bahari ya Hindi.
Data hizo kwa mara ya kwanza zilionyeshwa kwa ndugu na jamaa za
abiria waliokuwa ndani ya ndege ambao wamekuwa wakitaka uwazi zaidi
kuhusu taarifa hizo kabla ya data hizo kuwekwa hadharani kwa vyombo vya
habari.
Nyaraka hizo zilizoachiwa leo, zinajumuisha data zenye takribani
kurasa 47 ikiwa ni pamoja na maandishi kutoka kampuni ya Satelite ya
Uingereza ya Inmarsat.
Ndege ya MH370 ilipotea Machi 8 mwaka huu wakati ikisafiri kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria 239 wengi wakiwa raia wa China
ambapo hadi sasa haijapatikana na hakuna sababu maalum iliyotolewa juu
ya kupotea kwake.
0 comments:
Post a Comment