Nasra
akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee
ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba cha ICU hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu baada ya kufichwa
katika box kwa miaka 4 na mama yake mkubwa Mariam Said baada ya mama
yake mzazi kufariki mwaka 2010.
Hali
ya Narsa kwa sasa imezidi kutengemaa ,kunawili na kuonekana kama mtoto
mwenye nuru kama anavyoonekana tofauti na alivyookolewa kutoka katika
box siku tano zilizopita hapo mama huyo mlezi akimpatia chakula iana ya
wali na samaki anaopendelea Nasra.
Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa..
Petter
Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika
kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Morogoro. alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa
habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali.
SAKATA
la Mtoto aliyeishi katika box kwa miaka 4 sasa limechukua sura mpya
baada ya nyumbani kwa mama mkubwa wake Mariam Said kukutwa kuna shimo
kubwa lililojaa maji hali inayozidi kuwachanganya wakazi wa mjini hapa.
Wakiongea
na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa mtaa wa Azimio anakoishi
mama huyo , Tatu Mgagala alisema Mei 22 polisi walifika mtaani hapo
wakiwa na mtuhumiwa huyo na kukuta mlango umefungwa na kuamua kuvunja
ili waweze kuingia ndani kuangalia mazingira ya nyumba hiyo.
Alisema
baada ya kuingia ndani ya chumba cha Mariam walikuta kuna giza nene
kutokana na chumba hicho kuzibwa na mabox na hivyo kutoa mabox hayo .
Alisema
baada ya kutoa mabox hayo waliona shimo kubwa lenye maji karibu na
eneo lilipo box alikokuwa akiishi mtoto huyo na alipoulizwa mama huyo
kulikoni na kuacha maji ndani huku akijua kuna ugonjwa wa Dengue
alidai maji hayo huyatumia kunawa miguu na mikono usiku kabla ya
kulala.
‘’ Ndani ya nyumba hiyo sehemu zote zimesakafiwa isipokuwa eneo hilo ambalo lilichimbwa shimo hilo’’ alisema. Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo imebainika kuwa mariamu na mumewe kwa muda mrefu walikuwa hawajaoga na hivyo kulazimishwa kuoga wakiwa mbaroni .
Kwa
upande wake mtetezi wa haki za watoto Petter Mwita alisema
watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mei 26 mwaka huu ni Mariam
,mumewe Mtonga Omari na baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi.
Alisema
ndani ya nyumba ya mama huyo zikukutwa picha ambazo zinaonyesha kuwa
mtoto huyo alikzaliwa akiwa hana ulemavu na kwamba inadaiwa ulemavu huo
alipata kutokana na ukatili alikofanyiwa na walezi hao
‘’
Vitendo walivyofanya wote hawa watatu ni vya kikatili na vinatakiwa
kupigwa kwa nguvu zote nah ii itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye
tabia kama hii.
Alisema
baadhi ya mitandao ya kijamii ilivumisha kuwa mtoto huyo alinyanyasika
na mama yake mkubwa huyo kwa madai kuwa mama yake mzazi alikufa na
ugonjwa wa Ukimwi ambapo alisema suala hilo kwa mtoto huyo halipo kwani
tayari alishafanyiwa kipimo hicho na kubaini hana ugonjwa huo.
Hata
hivyo alisema kwa sasa wamemtafuta mama mlezi wa Mtoto huyo kwaajili ya
kumuhudumia katika huduma zote na anlipwa kwa kazi hiyo.
Naye
Josephina Joel mama ambaye kwa sasa ndiye anamlea mtoto huyo alidai
yeye amechukuliwa kutoka katika kambi ya kulelea wazee Fungafunga ya
mjini hapa na kwamba anajua uchungu wa watoto hivyo kwake anaona hakuna
changamoto zozote anazopata kwa mtoto huyo.
‘’
Mimi niliachwa na mume wangu naishi Fungafunga nalelewa na Ustawi wa
jamii kwangu kumlea mtoto huyo nachukulia kama mjukuu wangu na nafurahia
na sioni shida yeyote’’ Alisema.
Aidha
alisema mtoto huyo hupendela kula chipsi mayai, wali nyama au samaki
pamoja na juice huku akionyesha kukataa ugali wala maziwa.
Mtoto
huyo kama kitu hataki anafumba macho, kwa mfano ukimwambia nikupe ugali
anakataa, au maziwa , lakini pia hapendi kuoga na ukimwambia kuoga au
kula vyakula asivyotaka anakwambia badae’’ Alisema
Mwandishi
wa habari hizi alifanikiwa kufika nyumbani kwa Mvungi Kihonda eneo la
Maduka kumi anakoishi na mkewe wa ndoa kwa lengo la kutaka kujua jinsi
huyo mke alivyochukulia jambo hilo na kuwafukuza waandishi wa habari
kwa madai ya kuwa wakaandike wanavyojua wao.
‘’
Ehe waandishi wa habari mnataka nini tena kwangu uwiiii, mimi sijui
chochote, ondokeni, huku akiondoka kueleka sebuleni waliko mgeni wake
aliyemtmbulisha kama wifi yake huku akimwambia kwa lugha ambayo
ilisikika kwa neno lililoashiria wandishi wa habari hao’’ Alisema
Hata
hivyo waandishi wa habari walifika nyumbani hapo nao wakiwa nyuma
yake wakarudi naye hadi eneo alipo wifi yake na kujaribu kudadisi zaidi
jambo bila mafanikio zaidi ya kutawala kimya kwa muda wa dadki kumi na
ndipo alipoohoji tena kuwa wanataka nini.
Hata
hivyo mama huyo ambaye anaonekana ni mjamzito alionekana kupandisha
pumzi na kushusha hali iliosababisha kushindwa kuongea na hivyo
waandishi hao kuamua kuondoka kurejea mjini.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa alithibitisha kukamatwa kwa baba wa Nasra Said
na kwamba yuko nje kwa dhamana na aatafikishwa mahakamani pamoja na
watuhumiwa wezake Mei 26 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment