Taarifa ya picha kamili za Satelite kuhusu ndege ya Malaysia
iliyopotea MH370 zitatolewa kesho kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Kaimu waziri wa usafirishaji wa Malaysia Hishammuddin Hussein ametoa
taarifa kuhusu kutolewa data za ndege hiyo wakati akiwa anatembelea
kampuni iliyopo katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Familia na ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliyopotea
mwezi Machi mwaka huu ikiwa imebeba watu 239
katika eneo Kusini mwa
Asia wamekuwa wakidai data za ajali hiyo kuwekwa hadharani.
Hatma ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo bado imebaki kuwa moja ya kitendawili kikubwa kuwahi kutokea katika nyakati za sasa.
Kampuni ya Inmarsat, ambayo Satelite yake ilikuwa ikiwasiliana na
ndege hiyo iliyopotea katika dakika za mwisho imesema kuwa haikupewa
kibali na mamlaka za Malaysia kuachia taarifa hizo hadharani.
Lakini sasa kampuni hiyo na serikali ya Malasysia wanasema wanajaribu kufanya taarifa hizo zitolewe hadharani.
0 comments:
Post a Comment