Mgogoro
wa uongozi umezuka katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo wabunge wa
bunge hilo wanakusudia kumwondoa madarakani spika wa bunge hilo.
Tayari wabunge hao wameshakusanya saini 36 kutoka kwa wabunge 45 wa bunge hilo ambazo zinatakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Wabunge hao wanamlaumu Spika huyo kwa kukiuka kanuni za bunge pamoja kushindwa kuwashirikisha wabunge kwenye baadhi ya uamuzi.
Akiongea
na waandishi wa habari kiongozi wa wabunge hao kwa niaba ya wabunge
wenzake wa bunge hilo Abudulla Ali Hassani Mwinyi, amesema wabunge hao
wamefikia hatua hiyo ya kumwondoa spika huyo Margareth Zziwa kufuatia
kukerwa na mwenendo wake.
Tayari
wabunge hao wameshapeleka hoja ya kumwondoa spika huyo kwa Katibu wa
Bunge hilo ikiwa na sahihi za wabunge 36 ili kutimiza matakwa ya
utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo ili kuanzisha
hoja ya kumwondoa spika.
Je wabunge hao hawakuwa na njia nyingine kumaliza mgogoro huo hadi kufikia hatua ya kutaka kumwondoa spika huyo.
Mgogoro
huu wa uongozi ndani ya bunge hilo umesababisha kuahirishwa kwa bunge
hilo tangu jana kwa muda usiojulikana baada ya spika huyo kuamua
kuliahirisha kwa muda usiojulikana.
Hii inafuatia malumbano yalijitokeza ndani bunge hilo ambapo mmoja wabunge alisema hoja hiyo isingeweza kujadiliwa.
BBC
ilifanya juhudi za kuwasiliana na spika huyo Margareth Zziwa kwa simu
yake ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo hata hivyo alikataa kusema
chochote ambapo alishauri apigiwe afisa habari wa bunge hilo ili atoe
ufafanuzi.
Mgogoro
huu wa uongozi ndani ya bunge hilo bado haijajulikana utamalizika lini
lakini kwa vyovyote vile utakuwa umeathiri shughuli za Bunge hilo la
Afrika Mashariki.Chanzo BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment