Mgombea Ubunge katika Jimbo la Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ramadhani Mgaya (pichani juu) kupitia chama cha AFP amejeruhiwa kwa mapanga.
Mgaya
amesema amejeruhiwa na mtu mmoja akiwa na panga inasemekana kuwa huyo
jamaa aliyemkata mapanga mgombea huyo wa AFP alikuwa katika eneo hilo
kabla ya tukio maana naye alikuwa amepanga hapo ambapo chadema walikuwa
wamepanga GESTI HIYO NZIMA KUTOKANA NA HUDUMA NZURI ZINAZOTOLEWA NA
GUEST HIYO KWA UPANDE WA MALAZI NA VINYWAJI KULIKO GUEST ZOTE HAPO
CHALINZE na wakiwa wamefikisha siku kumi tangu walale hapo ndipo majira
ya saa sita za usiku wa kuamkia tarehe 4 mgombea
wa AFP alipoamua kulala hapa na kusababisha kutokuelewana na jamaa huyo
na kuanza vaarangati hilo wakati wakiwania chumba katika nyumba ya
kufikia wageni ya GOODTIME Chalinze iliyopo barabara ya Morogoro mita
chache kutoka njia panda(makutano ya barabara ya moshi,dar na moro).
"Nimevamiwa
na kujeruhiwa na mtu akiwa na panga aliyekuwa anataka kulala humu na
kutoweka kusikojulikana ila ahsante uongozi wa Chadema kwa kunisaidia,"
alisema Mgaya.
Mgaya amesema ameumia mikononi wakati akipangua nakujitetea maana mvamizi alikuwa na panga.
Mbali na yeye pia amesema kiongozi wa Chadema, Mwita Waitara naye
alijeruhiwa wakati wa purukushani za kumsaidia mgombea huyo wa chama cha AFP.
0 comments:
Post a Comment