Katibu
wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye sambamba na Mgombea Ubunge
katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya
Kikwete wakiyarudi magoma wakati wa Mkutano wa Kampeni za
CCM uliofanyika leo April 2,2014 katika Kijiji cha Lugoba,Kata ya
Lugoba.
Mgombea
Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani
Jakaya Kikwete akiwahutubia Mamia ya wakazi wa Kijiji cha Lugoba
waliofurika kwenye uwanja wa Mnadani,kusikiliza sera ya Mgombea Ubunge
huyo leo April 2,2014.
Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini,Stephen Masele akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lugoba wakati wa
Mkutano wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,leo April 2,2014.
Mbunge
wa Jimbo la Mchinga,Said Mtanda akihutubia wakazi wa Lugoba na wananchi
wa Chalinze kumchagua Ridhiwani Kikwete ili waweze kushirikiana nae
katika kuendeleza maendeleo ya Jimbo hilo.
Meneja
wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven
Kazidi akiwapa maneno murua kabisa wananchi wa Kata ya Lugoba na
kuwataka waache kwenda kujiunga na vyama vingine,kwani maendeleo ya kila
Mtanzania yanaletwa kupitia CCM.
Katibu
wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akihutubia Mkutano wa
hadhara wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
Bi.
Mwanahawa Omary aliekuwa Mwanachama wa Chadema akirudisha kadi kwa
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani
Jakaya Kikwete.
Mgombea
Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani
Jakaya Kikwete akiiangalia kadi ya CHADEMA ya Mzee Masoud Mtonga mara
baada ya kukabidhiwa.
Mgombea
Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani
Jakaya Kikwete akipokea kadi za Chama cha CUF kutoka kwa aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama hicho Kata ya Msata,Idd Njema ambaye amejiunga na
CCM sambamba na familia yake.katikati ni Meneja wa Kampeni za CCM katika
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kata ya Msata,Idd Njema akizungumza machache muda mfupi baada ya kujiunga na CCM.
0 comments:
Post a Comment