OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa Pastor John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye alinaswa akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama waumini wake kwa sababu wote ni Wakristo.
Pasta
John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance
lililopo Masaki, Dar baada ya kunaswa na wanawake watatu wakimchezea
utupu.
OFM YATONYWA UCHAFU WA PASTOR
Ilikuwa
Jumanne ya Aprili Mosi, 2014, saa 4:14 asubuhi, chanzo cha habari
kilipiga simu chumba cha habari cha Global na kuwataka makachero wa OFM
ambapo alipounganishwa nao alisema:
Pasta John Paul Simon Rubanguka akijaribu kujitetea.
“Huyu
pastor amempa dili dada mmoja kumtafutia wasichana wazuri watatu na
kuwapeleka kwenye nyumba moja hivi kisha wawe wanamchezea utupu wake
huku wao wakiwa kama walivyozaliwa, ndiyo furaha yake ilipo. Wasichana
wameshapatikana.”
Makamanda wa Polisi wakimbananisha na kumtuliza Pasta huyo ili apunguze munkari.
MSHIKO WA NGUVU NA SAFARI JUU
Mtoa
habari huyo aliendelea kudai kuwa, pastor huyo alisema wasichana
watakaokuwa wakichezea utupu atawafanyia usaili wa kwenda kuwauza kwenye
kasino moja iliyopo Uarabuni ambayo yeye ni wakala wa kuwapelekea
malaya huko.
Pastor akiwa na mmoja wa wanawake waliofumaniwa naye.
Chanzo hicho
kiliendelea kudai kuwa, pastor huyo aliwaahidi wanawake hao kitita cha
shilingi 300,000 kila mmoja kwa wale watakaofaulu kumchezea vizuri,
sanjari na kuwakatia hati za kusafiria ‘passport’.
Makamanda wa OFM wakimtuliza Pasta.
OFM YAWEKA MTEGO
Baada
ya kupata ishu nzima, OFM ilifanya ukachero na kugundua mahali ambapo
tukio hilo lilipangwa kufanyika, ni kwenye danguro moja lililopo
Kinondoni jijini Dar.
Wanawake walionaswa katika tukio hilo wakivaa viwalo vyao.
OFM
ilifika kwenye nyumba hiyo na kufanya ushushushu wake ambapo
walifanikiwa kuweka mitambo yao sambamba na kulishirikisha jeshi la
polisi kwa ajili ya kumnasa mtumishi huyo wa Mungu akifanya vitendo
hivyo.
Saa 8:11
mchana, OFM wakiwa wamejibanza eneo hilo waliwashuhudia warembo watatu,
weupe wakielekea kwenye nyumba ambayo mtoa habari wetu aliielekeza.
Kitambulisho cha Pasta.
PASTOR AWASILI KWA MBWEMBWE
Saa
11:23 jioni, OFM wakiwa hawajaanza hata kujisikia kuchoka, walimwona
pastor huyo akiwasili kwa mbwembwe akiwa ndani ya gari dogo na kugeuza
kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha akashuka. Mkononi alishika maji
makubwa. Alipokelewa na mmoja wa wanawake hao.
Bango lililopo Kinondoni Mkwajuni, Dar likieleza lilipo kanisa la Pasta huyo.
MCHEZO WAANZA
Saa
11:40 jioni, makachero wa OFM walifanya uchunguzi wa kina na kubaini
kuwa, tayari mchezo ulishaanza ambapo waliwataarifu polisi na kuungana
nao kwenda kuvamia nyumba hiyo.
Msafara
wa OFM na polisi hao ulifika nje ya chumba kilichokuwa kikidaiwa
kufanyika uchafu huo. Sauti ya muziki na wanawake waliokuwa kama wapo
kwenye darasa la siri zilisikika.
Polisi waligonga mlango na kujitambulisha kisha wakaomba wafunguliwe mlango haraka ndani ya sekunde chache.
PASTOR APATA MCHECHETO
Pasta
John na wanawake hao walitii amri kwa kufungua mlango ambapo mchungaji
huyo alikumbwa na mchecheto na kutaka kurukia juu ya dari lakini polisi
walimtafadhalisha kutulia pamoja na wanawake hao kama walivyo.
OFM ikiwa chumbani humo iliwashuhudia wanawake hao wakiwa watupu mbele ya pastor huyo ambapo walikuwa wakimnengulia viuno.
Baada
ya kupewa kibano, warembo hao walimwanika pastor huyo kwamba ndiye
aliyewatuma wamchezee wakiwa watupu ili awalipe shilingi laki tatu kila
mmoja, pia kuwapeleka Uarabuni kwenye kasino.
UTETEZI WA PASTOR
Kwa
upande wake, Pastor John alijitetea kuwa anaomba asamehewe kwa gharama
zozote ili taarifa hizo zisifike popote kwani ishu hiyo ilikuwa si amri
yake bali shetani alimpitia.
“Jamani
naomba tumalize humuhumu ndani, mnajua mimi ni Pastor wa Kanisa la
Maximum Deliverance, sasa ukweli ni kwamba waumini wangu hawatanielewa,
chondechonde ilindieni kazi yangu jamani,” alijitetea.
Mpaka
OFM inaondoka eneo la tukio, pastor huyo na wanawake ‘wake’ walikuwa
kwenye harakati za kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria kwa ajili ya
hatua zinazostahili.
KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI
Siku
zote kazi ya OFM ni kuwajibikia matendo maovu na si kuwaonea watu kwa
lengo la kuwachafua. OFM inapopata habari huichunguza ukweli wake kwanza
kabla ya kuchukua hatua ya kuifanyia kazi moja kwa moja, yaani kufika
kwenye eneo la tukio.
Lengo
kubwa la kutoa habari za aina hii ni kuwakumbusha watu namna ya kuishi
maisha yanayompendeza Mungu. Wengi wamebadilika, sasa wanaishi vizuri
wakiwa watu wapya na wanyenyekevu pia wenye kufundisha wenzao.
0 comments:
Post a Comment