Tuesday, March 25

 
Lingine ni kuonekana mwepesi kwenye suala la mapenzi hivyo mwanaume kuwa na mashaka kwamba hata kama akifikia uamuzi wa kukuoa unaweza kuwa mwepesi kutoa penzi kwa wengine kama ulivyofanya kwake.
Sasa hebu tuone athari anazoweza kupata msichana akiharakisha faragha na mwenzi wake.
 (i) Hupunguza thamani
Heshima ya penzi ni kwenye ndoa. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kushushwa thamani baada ya kutoa penzi. Wanaume wengi huanza kuwa wasumbufu (kama ni kasumba yao) kwa wapenzi wao baada ya kutoka nao kimapenzi.
Pamoja na kwamba ni tendo la furaha lakini kwa mwanamke linampa unyonge na wakati mwingine huwa mwanzo wa utumwa wa mapenzi kwa kuogopa kuachwa wakati tayari ameshatumika!
Hebu jiulize; utatumika na wangapi? Ukifikiri kwa makini juu ya jibu la swali hili bila shaka utabadilisha mtazamo wako.
(ii) Hupunguza msisimko
Penzi la kienyeji mara nyingi hata wahusika huwa wanajua kabisa kuwa wanakosea. Makosa haya husababisha kupoteza msisimko wa ndani. Ni jambo la kisaikolojia zaidi na huenda muathirika asigundue tatizo hili kupitia dalili za kitaalamu atakazozionesha.
Mkishaibana huko nje huwa kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupoteza msisimko wa kawaida. Mfano mawasiliano hupungua, hamu ya kuonana inapungua n.k
Hapa nisipoteze muda sana, wengi mnafahamu inavyokuwa; mwanaume akishatoka na mwanamke, taratibu ataanza kujiweka pembeni. Kama alikuwa anapiga simu mara nne au tano kwa siku, hupunguza idadi na wakati mwingine hupitisha siku nzima kabisa.
Mbaya zaidi, unaweza kumpigia wewe na bado asipokee, ukituma ujumbe mfupi hatajibu au atachelewa. Kesi nyingi sana nilizokutana nazo za wanawake wanaolalamika wapenzi wao kubadilisha utaratibu wa mawasiliano, baada ya kuwahoji walisema jambo hilo limejitokeza baada ya kuwapa penzi.

MUHIMU KWAKO KUJUA
Mwanaume wa aina hii ni yule ambaye hakuwa na mpango wa ndoa baadaye au hakuwa na uhakika na aina ya uhusiano anaotaka kwa mwanamke wake.
Sasa jiulize, ikiwa alikuwa kwenye majaribio, utajaribiwa na wangapi? Tumia hekima rafiki yangu ili kujinasua katika mtego huu.
(iii) Upungufu
Ukishautoa mwili wako kwa mwanaume, kama ni aina ya wale ambao huchunguza sana ni rahisi kukutoa kasoro. Utamsikia akisema: Aaah! Huyu mwanamke bwana ana sijui nini...hakuna hoja za maana.
Kikubwa unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba kuutoa mwili wako hovyo kunakupeleka kwenye kujichoresha na pengine kama umekutana na mwanaume kicheche ataishia kukutumia na kukuacha kama alivyokukuta!
(iv) Msimamo
Pamoja na kwamba wanaume wengi ndiyo hasa wanaokuwa wa kwanza kushawishi kupewa mapenzi, ukweli ni kwamba ni wepesi wa kulaumu (vipengele vilivyopita nilikazia zaidi) na kuwaona wenzi wao hawana msimamo na maisha yao.
Kukuweka kwenye kundi hilo kutakukosesha nafasi ya uhakika ya kuingia kwenye ndoa, maana wengi wanapenda kuwa na wenzi wenye msimamo thabiti.
 Kutokana na mabadiliko ya dunia, faragha imekuwa ni jambo la kawaida kabisa hata kwa wale ambao ni marafiki tu. Wanaofanya hivyo, huwa na imani kuwa wanawapagawisha wapenzi wao na kuwafanya wasifikirie kuwaacha.
Tendo la ngono limekuwa jambo la kawaida. Ni jambo ambalo linaweza kusababisha hata uhusiano kuvunjika. Siku hizi marafiki tu nao eti wanadai wana haki na tendo hilo.
Kiukweli ni kwamba tendo hilo hufanyika sana, ndiyo maana mada hii ikawepo ili kuwashtua vijana wajitambue na kushika utaratibu mpya. si vyema kuliacha jambo hili, kwa sababu linafanyika.
Hata hivyo, zipo athari zinazoweza kupatikana ikiwa tendo hilo litaharakishwa (maana lazima litafanyika). Wiki iliyopita nilianisha athari nne, leo tunamalizia mada yetu.
Kwanza nilieleza kwamba hupunguza thamani ya mwanamke, hupunguza msisimko, nikaelezea kuhusu upungufu na mwisho kupoteza msimamo. Sasa tumalizie.
(v) Mimba
Kuna suala la mimba. Nimekutana na kesi nyingi sana za aina hii. Wanaokutana kimwili na wenzi wao bila mpangilio huwa hawazingatii suala la mimba lakini inapotokea ndiyo huanza kuhangaika kutafuta ushauri.
Ndugu zangu, kama hujui hili, ngoja nikuambie, wanawake wengi wawapo faragha na wenzi wao huwa hawana ujasiri wa kuulizia kuhusu kinga.
Wanawake mara nyingi huwa hawanunui kinga wakati wakienda kukutana na wenzi wao. Ni kama vile anasikilizia mwenzi wake anavyotaka. Kama akitaka kutumia sawa, kama akikataa baasi!
Utafiti unaonyesha kuwa, wanawake wengi wanapokuwa faragha, akili na mawazo yao yote huwa katika kuwafurahisha wapenzi wao tu, mambo mengine huyapa nafasi ndogo sana. Hii ndiyo sababu hupata mimba bila kujiandaa. itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

-