Mtoto
aitwae Satrin Osinya ambae bado anarisasi kichwani mpaka sasa kutokana
na shambulizi lililofanywa kanisani Mombasa na watu wasiofahamika
Jumapili iliyopita ambapo mama yake mzazi aliuwawa.
Huyu aliembeba akiwa na huzuni inayoambatana na machozi ni Moses Gift
katika hospitali ya Coast General, Mombasa ambapo picha ya Xray
imeonyesha huyo mtoto bado ana risasi kichwani.
Imefahamika kwamba risasi iliyomuingia kichwani mtoto huyu ndiyo
iliyomuua mama yake, yani baada ya kunyooshewa silaha mama alikua ana
mkinga mwanae ndio risasi ikamuua yeye kisha ikaenda kutua kichwani kwa
mwanae.
Madaktari wamekuwa wakitazama picha za Xray na Scan kuchunguza iwapo
upasuaji utafanikisha kutolewa kwa risasi kichwani mwa Santrin bila
kumpa maumivu
au kuhatarisha maisha yake.
Santrin amekuwa akilia kwa uchungu alio nao kila wakati hospitalini
huku babake akitizama tu ashindwe la kufanya huku machozi ya kakake
Moses Gift mwenye umri wa miaka 13 yakiwaleta Wakenya kwenye taswira ya
unyama waliofanya magaidi wasiojali hata watoto.
Madaktari Mombasa wamekuwa wakijadili uwezekano wa kumsafirisha Santrin hadi jiji la Nairobi kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment