Tuesday, March 25

 
Mchumba wa Fariq Abdul Hamid, Nadira Ramli.
 
Mmoja wa rubani wa ndege ya Malaysia iliyopotea, Fariq Abdul Hamid.

 
 Nadira Ramli, Fariq Abdul Hamid walikuwa na mipango ya kufunga ndoa.
Mpenzi wa kike wa mmoja wa marubani wa ndege ya Malaysia iliyopotea Nadira Ramli amejichimbia katika hoteli moja jijini Kuala Lumpar na amewataka ndugu zake kutoangalia televisheni.
Fariq Abdul Hamid, 27, alikuwa amepanga kumuona msichana huyo ambaye pia ni rubani msaidizi katika ndege ya shirika jingine. Kwa sasa amepewa likizo ya mwezi mmoja ili kuiweka akili yake sawa wakati akisubiri matokeo ya ndege hiyo.
Taarifa juu ya uhusiano huo zilizovuja, zinasema kuwa rubani huyo aliyerusha ndege yenye namba MH370, ana uhusiano na kiongozi mmoja wa upinzani nchini Malaysia aliye jela.

Rubani huyo msaidizi anachunguzwa baada ya kuwepo kwa habari kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kusikika wiki hii muda mfupi kabla ya mfumo wa mawasiliano wa ndege hiyo kukatika.
Hamid alikutana na Nadira walipokuwa wakisoma pamoja chuo cha urubani katika shule ya Langkawi na wawili hao wamekuwa katika uhusiano kwa zaidi ya miaka tisa sasa
CHANZO: DAILYMAIL

0 comments:

-