Colonel
Mustapha ni miongoni mwa Wasanii wa longtime kidogo kwenye game ya
muziki Kenya toka enzi hizo akiwa kwenye kundi lililotoa hit single
yenye maneno ‘bibi yake mufupi, kijana murefu ametoka wapi’
Hivi karibuni ameingia kwenye vichwa vya habari sana hasa baada ya
kutangaza kuwa mapenzini na Huddah, mrembo aliewahi kuiwakilisha Kenya
kwenye shindano la Big brother Africa ambapo uhusiano wao hauchukua muda
mrefu ukavunjika.
Kabla ya kuvunjika, tayari walikua wameshapiga picha ambapo Mustapha
anasema alikua amerekodi wimbo na Huddah lakini walipoachana mrembo huyu
akasema Ogopa Dj’s wasiitumie tena sauti yake kwenye huo wimbo na kama
watafanya hivyo atawashitaki.
Hata hivyo picha zao wawili zilishasambaa kwenye internet tayari na kuanza kuchukua headlines kutokana na pozi zao.
Kuonyesha kupinga hiki kitendo, mwimbaji staa wa ‘watu na viatu’ Nyota ndogo aliungana na Wanawake wengine Mombasa na kuandamana kupinga kitendo cha Mustapha kuzisambaza picha zinazomdhalilisha Mwanamke hivyo aombe msamaha haraka iwezekanavyo.
Namkariri
Nyota akisema ‘Mustapha ambae ni msanii mkubwa ameanza muziki kitambo
kuchukua picha za watoto wa kike na kuwavua nguo, hii itanyima hata
Wazazi kuachia watoto wao kufanya muziki unaoonekana uhuni… ikiwa
Mustapha hatoacha hii itatuharibia, kama kaona ameshindwa kutunga nyimbo
zitazowashika watoto wa sasa hivi afate mtoto amuandikie’
‘Ameona jina linashuka ndio maana bora achukue picha za uchi
atengeneze skendo, Mustapha nimekua nae kwenye muziki miaka mingi, kwa
nini sasa hivi ndio afanye kwa sababu Prezzo anafanya? ama ameona Prezzo
yuko juu kwa sababu anafanya.. yeye ndio anatakiwa kumwambia Prezzo
usifanye hivi’
Hata
hivyo Mustapha amezungumza baada ya haya maandamano na kusema ‘Ni kitu
cha kushtua kuona maandamano yamefanyika kwa ajili ya Mustapha, wakati
tunapiga hizi picha hakukua na lengo lolote la kumdhalilisha Mwanamke
bali ilikua mambo yetu yenyewe kwa raha zetu, nilivyoona youtube kuhusu
haya maandamano nimehuzunika… naomba msamaha kwa yeyote aliekerwa na
hili… nimekubali kuomba msamaha kwa Wanawake’
Kwa kumalizia Mustapha amesema ‘kuna Wasichana ambao wanataka tupige hizo picha na wananilipa’
0 comments:
Post a Comment