Saturday, December 14


Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea akionesha kitabu cha The Birthday Party cha  mshindi wa pili wa tuzo za Burt katika mzunguko wa tano kilichoandikwa na Mukama Mwijarubi,  kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw. Ramadhan Ali.
 
Lugha ya Kiswahili ni lugha yetu pendwa ya taifa ambayo kila siku kadri siku zinavyokwenda inazidi kujizolea sifa kemkem na kuzidi kujipatia wazungumzaji wengi barani Afrika,ambapo kwa takwimu za hivi karibuni inaonyesha kuwa Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 50.
Kuhusu elimu, nchi zote tatu za Afrika Mashariki zimechukua hatua mbalimbali muhimu kuipatia lugha ya Kiswahili nafasi katika mifumo yao ya elimu. Katika hilo, nchi ambayo imepata mafanikio makubwa, ikilinganishwa na zingine, ni Tanzania. Pamoja na ukweli huo, kinyume na imani ya baadhi ya watu, mafanikio ya Kiswahili katika elimu nchini humo hayakupatikana kwa urahisi.
 Hili limeelezwa kwa muhtasari na BAKITA (1999). Kufikia wakati wa kupatikana uhuru kutoka kwa mkoloni, lugha ya Kiswahili ilikuwa imeibuka wazi kama lugha inayotumika na wengi, na ikateuliwa kuwa lugha ya taifa mwaka 1964 na hatimaye ikateuliwa kuwa lugha rasmi pia. Mwaka wa 1967, iliamuliwa kuwa itakuwa lugha ya kufundishia elimu yote ya msingi, na 1970 ikaanza kutumiwa katika vyuo vya walimu wa shule za msingi.


 Matarajio yalikuwa kwamba hatua hii itapanuliwa na kujumuisha shule za upili na hatimaye vyuo vikuu. Lakini kufikia mwaka 1984, serikali ilisema kuwa Kiingereza kingeendelea kutumika. Wizara ya Elimu na Utamaduni ilisema wazi tena mwaka 1995 kuwa Kiingereza kiendelee kutumika. Licha ya Ripoti ya Tume ya Rais ya Elimu ya 1982 (Tume ya Makweta) kushauri kuwa Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia elimu ya juu nchini Tanzania (shule za upili 1985 na vyuo vikuu 1992), hakuna lililofanyika hadi sasa.
 Hii yote tukubali tukatae inatokana na ukweli kuwa lugha ya Kiswahili bado inakuwa na haijakidhi viwango stahiki kuweza kutumika katika mawasiliano kimataifa na ndiyo maana hata serikali ikaliona hilo na kuona umuhimu wa kuzidi kuhimiza kuhusu kujifunza lugha ya kiingereza katika shule za upili ili Kuhakikisha uthabiti, ubora na ufasaha katika mawasiliano ya kimataifa na nikiri kuwa lugha ina nafasi muhimu sana.
  Sambamba na hilo pia ndiyo maana hata waziri mwenye dhamana na elimu nchini mheshimiwa Shukuru Kawambwa akafikia maamuzi magumu ya kuanzisha mfumo wa mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa shule za msingi na upili nchini mwezi may mwaka huu kwa kushirikiana na serikali ya uingereza BRITISH COUNCEL na shirika la VCO ambapo kwa pamoja waliafikiana kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa wanafunzi na wananchi wote wanakuwa na uelewa na lugha hiyo ya kiingereza.
Wakati wa uzinduzi huo mh.kawambwa alikiri wazi kuwa asimia 95 ya wanafunzi wa shule za upili nchini hawajui lugha hii ya kiingereza na niseme kuwa sasa umefika wakati wa kuacha mawazo mgando tuliyonayo wengi wetu na kuanza kujifunza lugha hii ambayo naweza kukiri kuwa ni lugha ya dunia kwasasa ku
  Na ndiyo maana sasa,MRADI WA VITABU KWA WATOTO nao umeona haja pia ya kuunga mkono jitihada hizo ili kuweza kushindana na si kushindana tu bali na kuleta ushindani katika Nyanja mbalimbali za kidunia zitakazokua zikiandaliwa kwani lugha hii ya kiingereza ndiyo lugha kuu ambayo hutumika katika kuwasiliana kimataifa.
 Imefika wakatio sasa kwa kushirikiana na mradi huu wa vitabu kwa watoto uwe mwanga katika kujifunza lugha ya kiingereza na kuacha kasumba na lawama ambazo kiukweli hazina manufaa ya kiushindani katika dunia ya sasa.Mradi huu wa vitabu kwa watoto ni mradi unaoendeshwa kwenye nchi za Kenya,Tanzania,Ghana,Ethiopia na Uganda lengo kuu likiwa ni kukuza uelewa na ufahamu wa lugha ya Kiingereza ncini na pia kuibua vipaji vipya vya uandishi wa riwaya kwa watoto wa umri wa miaka 10-15 lengo likiwa ni kuwajengea msingi mzuri tangu wakiwa wadogo.
 Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mkurugenzi mtendaji wa mradi wa vitabu kwa watoto Tanzania Bi.Pilli Dumea amesema kuwa waliamua kuwa na mradi huo kwa lengo la kuungana na wizara ya elimu nchini katika kuhakikisha kuwa wananchi hususani watoto wa Kitanzania wanakua katika ufahamu wa lugha ya kiingereza ili kuweza kuleta na kukabiliana na ushindani katika Nyanja za kimataifa ambapo kwa kipindi kirefu watanzania wameshindwa kuwepo katika ushindani huo kwa sababu ya uelewa ama kutokujua kabisa lugha zinazotumika kimataifa hususani kiingereza.
   “zaidi ya asilimia 95 ya wanafunzi wa elimu ya msingi,elimu ya upili na elimu ya juu hawafahamu lugha hii,ni jambo la kushangaza kiukweli na inabidi kuchukua hatua sasa kuondokana na aibu hii kwani kama mwanafunzi wa chuo kikuu hafahamu lugha hii na wakati mameisoma tokea shule ya msingi si jambo zuri hata kidogo”alisema.
   Mradi huo ambao unadhaminiwa na kuendeshwa  na mcanada Willium Boots umekuwa ni mradi endelevuna mpaka kufikia sasa umekwisha waibua na kuwajengea uwezo kama siyo mwanga katika vipaji vyo zaidi ya watanzania 50 na kwasas wamezindua rasmi mashindano hayo kwa awamu ya sita nchini.
  Lengo kubwa na la msingi kwa mradi huu ni kuibua na kukuza vipaji kwa waandishi wa riwaya vilevile kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania inakwenda na wakati uliopo kwa kuhakikisha kila mara wanachapa au wanaandaa muswada wa vitabu vya hadithi na riwaya ili viweze kutumika nchini kwa wanafunzi wa shule za msingi.
  Bi Dumea anasema.”ni wakati sasa wa kuacha kasumba tuliyokuwa nayo,tokea mimi nasoma mwaka 69[1969]hadi leo vitabu vinavyotumika vya kujifunzia mashuleni ni vile vile jambo ambalo linapelekea kwamba kutokuendana na maisha halisi ya wakati huu kwa watanzania.kwa kuliona hilo tuna hakika kuwa miswada tutakayoipata katika mashindano haya itaondoa changamoto hii inayoikabili Tanzania yetu na wanafunzi wa wakati huu”alimalizia.
Ni jambo la kufurahisha na linalotia matumaini katika muelekeo wa elimu yetu nchini na hili litafanikiwa tu endapo juhudi za ziada na ushirikiano wa kutosha katika kuyatimiza haya ya taasisi hii ya vitabu kwa watoto.kwani hakika kwasasa watoto wetu mashuleni watakuwa na mwanga na vitendea kazi ambavyo vitasaidia katika vita hii ama jitihada hizi za serikali na wizara ya elimu katika kuhakikisha kuwa elimu na ufahamu wa lugha ya kiingereza unakuwa mkubwa nchini kwetu na kuwaandaa vijana na wasomi wetu kuingia na kuleta ushindani katika Nyanja ya kimataifa na kuleta ubora zaidi wa elimu yetu.
   Mbali na zawadi watakazopatiwa washindi wa uandikaji wa miswada hiyo ya riwaya chini ya mradi huu,pia mradi huo kwa kushirikiana na serikali na wizara husika huchapa miswada ile yenye ubora unaolingana na masharti ya uandikaji na ushiriki wa mashindano hayo hutumika katika mitaala ya elimu ya msingi kwa watoto wa shule za msingi nchini na katika maktaba mbalimbali nchini.
  “mfano mzuri ni washindi wa mashindano ya raundi ya tano bwana Richard mabala aliyeshinda na muswada wa riwaya yake ya run free na Israel Yona aliyeshinda na muswada aliokuwa akiuita tears from lonely heart tayari tumeanza kushirikiana na kampuni ya kuchapa na muda sii mrefu vitapatikana mashuleni na kwenye maktaba zetu na maktaba mbalimbali nchini Tanzania.
   Akijibu swali la changamoto wanazokumbana nazo katiak kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea bi Dumea anasema”changamoto yetu kubwa ni ufahamu mdogo wa lugha hii nchini hali inayopelekea hata kukosekana kwa washiriki wa kutosha katika shindano hili kwani wengi wao hushindwa kutokana na kipengele cha lugha ya kiingereza,jambo hili ni kubwa sana kwetu sisi kwani ukilinganisha washiriki wa Kenya na Tanzania,Kenya wamepiga hatua kwa kuwa na washiriki zaidi ya 500 japo wameanza mashindano msimu huu na sisi[watanzania] hatufikii hata robo ya washiriki wao”alisema
   Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka nchini,mshindi wa kwanza kwa msimu huu atapata million 17,wa pili milioni 14 na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha shilingi milioni 9 za kitanzania.
Mfano mwingine mzuri ni kwa msanii Ramsey wa Nigeria alipokuja Tanzania,alisema hivi nanukuu “Nimetembea na kujifunza mengi wasanii wa Tanzania wengi tuna vipaji vya hali ya juu katika uigizaji lakini inawezekana tatizo letu lipo katika soko letu kwa kazi zetu, nimeongea na mwigizaji wa kimataifa kutoka nchini Ghana Van Vicker amenishauri umuhimu wa wasanii wetu kujua Kiingereza ikiwezekana kurekodi hata filamu itakayotumia lugha hiyo,”anasema Ramsey.
  Naamini utakuwa umepata mwanga wa kutosha juu ya umuhimu wa kushirikiana na mradi huu wa vitabu kwa watoto nchini,tuwape ushirikiano wa kutosha vijana wa chuo mjitokeze kushiriki kwa wingi na wadau wote pia tushiriki kwani shindano hili ni kwa watanzania wote na kwa kufanya hivyo tutafanya jambo katika kuikomboa elimu yetu na kuwasaidia watoto na wadogo zetu waliopo mashuleni.kwa leo nawekea nukta hapa.
                KEVIN R.LAMECK.
+255 769 91 29 31
+255 654 61 33 26

0 comments:

-