Saturday, December 14

                Pix 01 - Copy

       " VIONGOZI WAKUU WA MRADI HUO"

Mradi wa vitabu vya watoto Tanzania umezindua  shindano la uandishi wa riwaya za Kiingreza kwa ajili ya kuwajengea msingi wa kujifunza kwa urahisi lugha hiyo vijana hapa nchini.
Shindano hilo ni sehemu ya tuzo ya Burt ya fasihi ya kiafrika iliyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2008 na kwa mwaka huu ni mzunguko wa sita wa mashindano ya uandishi wa riwaya za kiingereza kwa ajili ya vijana .


Akizindua shindano hilo leo(jana) jijini Dar e salaam Katibu Mtendaji wa Mradi huo Bibi Pilli Dumea amesema kuwa  lengo la mashindano hayo ni kuatambua kazi nzuri zinazofanywa na waandishi wa fasihi barani Afrika na kuwahamasisha waandishi wachanga waweze kushiriki katika ujenzi wa fasihi .
"BAADHI YA WAANDISHI TUKIFUATILIA UZINDUZI HUO"
“Lengo la mashindano haya ni kutoa changamoto kwa waandishi  na wasomaji wa riwaya za kiingereza wa hapa nchini na Afrika kwa ujumla ili kuongeza kasi ya usomaji  na uandishi wa riwaya za kiingereza ili kuongeza uelewa wa lugha  hiyo”, alisema Bibi. Pilli.
Aidha aliongeza kuwa mashindano haya yatakuwa na ushindani mkubwa kwani yanashirikisha washiriki toka nchi nne ambazo ni wenyeji Tanzania, Ethiopia, Ghana  pamoja na Kenya.
“Mashindano haya ya mzunguko wa sita yatakuwa na ushindani sana na zawadi ya mzunguko huu ni dola za kimarekani elfu tisa kwa mshindi wa kwanza, dola elfu saba kwa mshindi wa pili na dola elfu tano kwa mshindi wa tatu”, aliongeza Bibi Pilli.
Alisema kuwa mwisho wa kupeleka muswada wa riwaya itakuwa mwakani Mwezi Mei na muswada huo unatakiwa uwe na maneno yasiyozidi elfu 20 na yasizidi elfu 40.
Muswada huo unatakiwa uwasilishwe kwa Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania katika barua pepe yao ya childrensbook@gmail.com au nakala katika ofisi zao.

0 comments:

-