Mkurugenzi wa mafunzo (AJTC) mwenye koti jeupe akiwa pamoja na baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho wakisikiliza kwa makini moja ya mada za ujasiriamali zilizotolewa chuoni hapo hivi karibuni |
· Jumla ya wanachuo 227 wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wanatarajiwa
kushiriki katika mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za ukuzaji wa biashara,
yatakayotolewa na wakufunzi wa chuo hich
Baadhi ya wakufunzi wa AJTC wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiriamili iliyokuwa ikiendelea chuoni hapo |
Akizungumza
na blog hii mratibu wa
mafunzo hayo Bwana Andrea Ngobole amesema kuwa: mafunzo hayo yatakuwa
ya siku mbili
kuanzia tarehe 19-20/09/2013na yanalenga kuwapa wanachuo hao juu ya
mbinu na maarifa kuwa wajasiriamali na wafanyaiashara wenye mafanikio
na kuwa chachu ya maendeleo kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla
· Amesema kuwa kitengo cha ujasiriamali
chuoni hapo kimekuwa kikiandaa semina za ujasiriamali kwa wanachuo hao kila
mwaka na kwa mwaka huu kinatarajia kuwasilisha mada 7 kutoka kwa watoa mada
wanne ambao pia ni wakufunzi wa chuo hicho.
· Semina hii itajumuisha mada kama
Business Ventures, Business Networking na Business Family zitakazo wasilishwa na
Neema Mwaipela pia kutakuwa na mada ya kutathimini biashara na misingi 10 ya
ujasiriamali itakayowasilishwa na Ngobole pia Cash Flow Quadrant
itakayowasilishwa na Adson Kagiye. Alisema Bw. Ngobole.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari arusha Ajtc wakifuatilia kwa makini moja ya semina za ujasiriamali zilizowahi kuendeshwa chuoni hapo |
Ngobole amesema semina hiyo itatanguliwa na mada ya ufunguzi wa
semina hiyo itakayowasilishwa na mgeni rasmi Bwana Joseph Kagiye
Mayagila ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa mafunzo wa chuo cha
uandishi wa habari na utangazaji Arusha ( AJTC )
·
Ameyataja
madarasa yanayotarajiwa kushiriki katika semina hiyo kuwa ni
MKOMANZI, TANGANYIKA, SERENGETI, UDZUNGWA, RUWENZORI,
KILIMANJARO, MANYARA, NYASA, KITENGO CHA ELIMU NA KOMPYUTA. na madarasa
yaliyopo likizo kama SELOUS, NATRON RUAHA yataandaliwa semina mara
watakaporejea kutoka likizo mnamo october au november kulingana na
ratiba itakayotolewa na idara ya taaluma chuoni hapo
0 comments:
Post a Comment