Sunday, August 11

WATU wengi wanapenda kuwa maarufu, wenye uwezo na ushawishi katika jamii lakini hawafahamu wafanye nini kufikia ndoto zao. Kuna wanaolazimika kufanya hata mambo machafu mfano kupiga picha za utupu wakiamini zitawasaidia kujulikana.
Mfumo wa kufanya kitu chochote ili uwe maarufu si mzuri; zipo mbinu za kitaalamu ambazo mtu akizitumia anaweza kuwa maarufu na mwenye mafanikio makubwa katika jamii. Nazo ni hizi hapa.
Hakikisha ujuzi wako haumfuniki mkuu wako au watu wengine
Unaweza usiwe ujuzi pekee lakini hata uwezo wako wa kiakili, mali na uelewa. Hakikisha hauutumii kwa majivuno kuonesha jinsi unavyowazidi wenzako kazini, kwenye biashara, darasani hasa watu waliokuzidi cheo. Siku zote hakikisha kuwa unawatanguliza wenzako, kuthamini mchango wao na kusifu uwezo wao.
Kizuizi kikubwa kabisa kwenye maisha ya umaarufu, heshima na mamlaka kwenye jamii ni kujiona bora kuliko wenzako, jambo linalowafanya watu pamoja na uwezo wao washindwe kuheshimika na kupendwa.
Usiwaamini mno marafiki, jifunze kuwatumia maadui zako.
Jihadhari na marafiki, kwani wanaweza kukusaliti haraka zaidi kwani ni rahisi sana kwao kukuonea wivu. Watu hao ni rahisi sana kubadilika na kuwa katili. Ukianzisha uhusiano na mtu ambaye aliwahi kuwa adui yako, utagundua kwamba atakuwa mwaminifu zaidi kwako kuliko rafiki, kwani anakuwa anataka kukuthibitishia kwamba uhusiano wenu ni wa dhati. Kwa kifupi, waogope zaidi marafiki zako kuliko maadui.
Katika safari ya kuelekea kwenye kilele cha umaarufu na heshima, kuwa na maadui ni jambo muhimu kwani husaidia kuongeza ari na huthibitisha uwezo wako hasa pale inapotokea maadui zako kusalimu amri kwako.
Dhamira zako zifanye siri
Hakikisha watu hawakuelewi kwa dhamira zako au sababu ya kile unachokifanya. Kama hufahamu nini unataka kukifanya, ni dhahiri watakuwa hawana nguvu ya kukufanya lolote. Hakikisha unawapotosha wasijue mipango yako na wakati watakapofahamu dhamira yako, watakuwa wamechelewa kwani utakuwa tayari umeikamilisha mipango hiyo.
Epuka kuwa mtu wa kuropoka juu ya madhumuni yako ya maisha, utawapa nafasi wabaya wako kukuwekea vikwazo vya kukuzuia usifike mahali ulipokusudia.
Usipende kuzungumza sana
Unapotaka kuwavutia watu, punguza wingi wa maneno yako, kusema sana kunaweza kuwafanya wanaokusikiliza wakakukinahi.  Watu maarufu huweza kuwavutia na kuwaogopesha watu kwa kusema maneno machache.  Jinsi unavyozungumza zaidi, ndivyo unavyojenga uwezekano wa kusema kitu cha kipumbavu kitakachokudharaulisha.

Hakikisha unalinda hadhi
yako katika jamii
Hadhi katika jamii ndiyo nguzo ya mamlaka. Kwa kutumia hadhi yako pekee unaweza kuwaogopesha watu na ukafanikiwa mambo yako; lakini ukipotoka tu, fahamu umeingia matatani na utashambuliwa kutoka pande zote.  Hakikisha hadhi yao inabaki imara.

Itaendelea wiki ijayo...

0 comments:

-