Tuesday, July 23


 Msanii chipukizi wa Bongo Muvi nchini Gado Balotel  akiwa mwenye huzuni baada ya kuvunjika kiuno na miguu yote.

  Hapa kama inavyoonekanamiguu ya  Gado Balotel  na bandeji baada ya kuvunjika yote mara baada ya kujirusha toka ghorofa ya 5
  Mshare unamuonesha  Gado Balotel  akiwa kwenye kava la moja ya filamu zake alizocheka kabla ya kukumbwa na balaa hilo.
 Msanii na Kiongozi wa kundi la Bongo Muvi nchini JB ambae ameombwa na wasanii kuchangisha harambee haraka ili kupata fedha za kumsadia msanii mwenzao huyo anaeishi kwa mateso makali.
  Msanii na mwanamasumbwi wa zamani Fike Wilson ambae amepongezwa na wadau baada ya kujitolea kumsaidia msanii huyo, ambapo kwa sasa anaishi nyumbani kwa Fike huku akiwa anabebwa kupelekwa chooni na kurudishwa pia.
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Saimon Mwakifwamba nae pia ameombwa kuungana kwa pamoja na wasanii wengine kumsaidia msanii mwenzao anaishi kwa mateso makubwa usiku na mchana.

Msanii nyota toka kiwanda cha muvi za kibongo nchini Maulidi Mfaume maarufu kwa jina la Gado Balotel sasa amekumbwa na balaa la aina yake baada ya kuvunjika miguu yote miwili pamoja na nyonga kuteguka baada ya kudondoka toka ghorofa ya nne alipokuwa akiigiza filamu ya msanii mwingine aitwae Baga.

 

Baada Xdeejayz na kituo cha luninga cha DTV kupata taarifa hizo lilipiga hatua ndefu hadi mahala anapojiuguzia msanii huyo ambako ni nyumbani kwa msanii Wilson Fike maeneo ya Home Alone Vijana Kinondoni na kuonana uso kwa uso na msanii huyo aneishi kwenye maumivu makali.

 

Akiongea na mwandishi wetu nyumbani hapo Balotel alisema alikutwa na balaa hiyo wiki mbili zilizopita akiwa Location ndani ya hotel ya Con Way iliyopo Magomen Kagerana wasanii wenzake kama Hemed, Baga, Manaiki Sanga na wengineo wakati wakiigiza.

 

Balotel aliendelea kusema kuwa wakati shughuri za kuigiza ziliendelea na kuna sini moja iliyokuwa inahitajika kuigizwa kwa mfano ikimtaka mtu aigize kama anataka kujirusha kwenye ghorofa lakini asiruke ili kameraman  kuchukua picha achukue shoti hiyo kisha mtu huyo aende chini kisha achukuliwe shoti nyingine ya kujifanya ametua chini.

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa nafasi hiyo ilibidi aigize msanii mwenye filamu Baga lakini kutokana na uwoga wa msanii huyo alikuwa akijishauri namna ya kuigiza kuruka ghorofani ndipo Ballotel akamtoa pembeni na kumuonesha namna ya kuruka kama Jet Lee huku akimwambie mwenzake hiyo ilikuwa kazi ndogo sana.

 

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa baada ya hapo alijikuta ameruka toka ghorofa ya nne, lakini aliendelea kusema“ Wakati nikiwa bado sijashuka chini njiani nilianza kuhisi harufu ya kifo kwani tayari nimuona Israel mtoa roho akinipungia mkono na hatimae nilitua chini  kwa kufikia miguu” Alisema  Ballotel

 

Hata hivyo kijana huyo aliongeza kusema kuwa mala baada ya kutua nchini alihisi moto unawake miguuni mwake huku harufu ya damu ikimtoka puani na mdomoni na baada ya kujiangalia aliona visigino vyake vikiwa vimepasuka vyote huku tumboni kukiwa na maumivu makali sana kumbe wakati huo nyonga ilikuwa imeachia huku miguu yake ikiwa imesogea tumboni.

 

Gado alisema baada ya tukio hilo wasanii wenzake walimchukua na kukmimbiza Hospital ya Mwananyamala mbapo dakika chache baadae walimkimbiza Muhimbili kwa matibabu zaidi.Msanii huyo ambae ametamba sana kwenye filamu kama Going Bongo,Msitu wa Hifadhi,Tumbo Joto na Escap ambayo alikuwa akiigiza siku ya tukio lililomkuta.

Aidha msanii huyo aliendelea kusema kwa sasa anaishi kwenye mateso makali huku wasanii wenzake wakishindwa kumpa ushirikiana “Hapa nilipo nalelewa na Fike Wilsoni ndiye anaenibeba kwenda chooni na kunirudisha kwa kweli hali yangu sio nzuri nahitaji msaada wa wasanii wenzengu, Wako wanaokuja kunirushia chochote kama

 

Kalapina,Young Killer na madaktari wanasema huenda wakanishauri kwenda India ili wakazirekebishe nyonga zangu” Alisema Gado na kuongeza kuwa anawaomba wasanii wenzake wasamalia wema kumsaidia kwani hali yake ni mbaya na huenda kwa mujibu wa madakatari wake akahitajika kupelekwa India ili kukinusuru kiuno chake la sivyo hatozaa tena kwa vile nyonga vimeshafyatuka.

 

0 comments:

-