PABLO NI NANI?
Katika milima
inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya
kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya
yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya
watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni
gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa
Colombia.
Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza yote
ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya
serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe.
Si hivyo tu, bali hata maaskari magereza ambao walikuwa wanalinda
gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya
Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogolea gereza hilo hata umbali wa
maili 12. Kama hiyo haitoshi gereza hili lilikuwa na uwanja wa mpira wa
miguu, lilikuwa na bafu lenye Jaccuzi, lilikuwa na bar, lilikuwa na
maporomoko ya maji (water falls) yaliyobuniwa kiustadi, na pia chumba
(selo) alicholala mfungwa huyu kilikuwa na kitanda kikubwa cha duara
chenye kuzunguka pamoja na televisheni kubwa.
Kama hii haitoshi
kwenye gereza hilo pia kulikuwa na chumba maalumu cha michezo ya watoto
maalumu kwa ajili ya watoto wa mfungwa huyo pindi akitembelewa na
familia yake. Na pia ndani ya gereza kuliwekwa darubini kali (Telescope)
ya kumuwezesha mfungwa huyo kuangalia katika mji wa Medellín ambako
familia ya mfungwa huyu iliishi na kila siku jioni walitoka nje
kibarazani kuongea naye kwenye simu huku akiwatazama kwa darubini.
Gereza hili lilijulikana kama La Catedral (the cathedral) na
lilimuhifadhi mfungwa muhimu zaidi duniani na binadamu aliyeifinyanga na
kuifanya biashara ya mihadarati iwe jinsi ilivyo hivi leo. Marafiki
zake wa karibu walipenda kumuita El Patrón (The Boss) au El Zar de la
Cocaína (The Tsar of Cocaine) lakini alipozaliwa wazazi wake walimuita
Pablo Emilio Escober Gaviria au kwa kifupi Pablo Escobar kama ulimwengu
wote ulivyomtambua.
The Boss
Akiwa mtoto wa tatu kwenye
familia ya watoto saba ambapo baba yake alikuwa ni mkulima na mama yeke
mwalimu wa shule ya chekechea, Pablo Escobar alikuwa ni mwenye kutamani
mambo mazito na mwenye maono makubwa tangu angali mtoto.
Akiwa
bado kwenye umri wa makumi (teenage) Pablo mara kwa mara aliwaambia
ndugu zake na marafiki zake kuwa anataka awe na utajiri wa kiasi cha
Peso Milioni 1 za Colombia (COL$ 1 Million) atakapofikisha umri wa miaka
22.
Ndoto hizi zilimfanya ashindwe kumaliza Chuo kikuu alipokuwa
anasoma (Universidad Autónoma LatinoAmericana of Madellín) na
kujiingiza katika biashara za halali na haramu na hatimaye aliacha
masomo chuoni. Moja ya biashara zake haramu za kwanza kabisa akiwa
kijana chini ya miaka 21 ilikuwa ni kutengeneza vyeti bandia vya
stashahada vya chuo alichokuwa anasoma na kuwauzia watu waliohitaji kwa
ajili ya kwenda kupata ajira.
Pamoja na biashara hiyo pia Pablo
alijihusisha na kusambaza mizigo ya sigara zilizokuwa haziruhusiwi
nchini Colombia (Marlboro), pia alifanya kazi kama mlinzi binafsi
(bodyguard) pamoja na wizi wa magari.
Moja ya matukio muhimu ya
ujana wa Pablo yaliyochangia kuamsha ari ndani yake na kumfanya atamani
kuwa moja wa manguli wa biashara haramu lilikuwa ni tukio ambalo
alipofikisha miaka 26 alifanikiwa kuweka benki (Cash Deposit) kiasi cha
Peso Millioni 100 za Colombia (COL$ 100 Million).
Mafanikio haya
yaliwasha taa ndani yake na kuamsha ari ya kutaka kuwa ‘Papa’ katika
‘Dunia’ ya siri ya ulimwengu wa biashara haramu.
Katika miaka ya
1970 mamlaka ya kupambana na matumizi mabaya ya madawa nchini marekani
(US Drug Enforcement Agency) waliwahi kutangaza kuwa wamewekeza zaidi
rasilimali zao kupambana na matumizi na uingizaji wa dawa aina ya Heroin
nchini marekani na kwa maoni yao walisema kuwa wanadhani madawa aina ya
Cocaine hayakuwa na uwezo wa kuleta uteja (addiction) au kufanya
mtumiaji kuwa muhalifu tofauti na dawa aina ya Heroin. Hivyo basi
walielekeza nguvu zao zote na rasilimali kupambana na biashara ya
usafirishaji wa Heroin kama kipaumbele cha kazi zao.
Hili
lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa upande wao. Kwani kijana Pablo aliona
mwanya huu na udhaifu huu upande wa DEA au pengine tusema kwamba Pablo
alifahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa mihadarati kuliko DEA.
Kitu
kikubwa ambacho Pablo alikiona na watu wakiwemo DEA hawakukiona ilikuwa
ni uwezekano (potential) ya kuifanya Cocaine kuwa moja ya madawa yenye
soko zaidi Amerika ya Kaskazini. Katika kipindi hiki kulikuwa na
watumiaji wachache sana wa Cocaine nchini marekani lakini Pablo aliona
fursa ya kuifanya mihadarati hiyo kuwa moja ya madawa yenye kuhitajika
sana nchini marekani na ulimwenguni kiujumla.
Kutokana na uzoefu
wake wa ulimwengu wa kihalifu, Pablo aligundua kuwa zao la Coca
linalimwa nchini Bolivia ambalo linatumika kutengeneza Cocaine ni bora
zaidi kuliko Coca inayolimwa nchini kwake Colombia. Hivyo basi Pablo
akadhamiria kuwa kama anaingia kwenye biashara hii ya kusafirisha
Cocaine ni lazima mihadarati yake iwe tofauti na bora zaidi kuliko
Cocaine nyingine watu waliyozoea kutumia. Akadhamiria kufanya Cocaine
yake iwe daraja la kwanza ili kuvutia watumiaji na kufanya soko likue
kwa haraka.
Kama sehemu ya mkakati wake wa kuingia rasmi kwenye
biashara ya kusafirisha mihadarati aina ya Cocaine, mwaka 1975 kijana
Pablo alisafiri mpaka nchini Bolivia kukutana na Roberto Suaréz Goméz
ambaye marafiki zake walipenda kumuita El Padrino (The Godfather)
kiongozi wa Genge lililoitwa La Corparacíon (The Corporation). Suaréz
alikuwa ndiye mtu pekee anayeendesha na kuratibu uzalishaji wa zao la
Coca katika nchi ya Bolivia na Peru. Kipindi hiki Suaréz tayari alikuwa
na mtandao mkubwa katika America ya kusini na alikuwa na jina kubwa,
ushawishi na nguvu ya kijeshi hivyo haikuwa kazi rahisi kwa kijana Pablo
kumshawishi Suaréz akubali kufanya naye biashara.
Huyu bwana
Suaréz alikuwa na nguvu kiasi kwamba alikuwa na jeshi lake binafsi la
anga (Air force) na wanajeshi wa miguu 1,500 ambao walipatiwa mafunzo
nchini libya.
Pablo alitumia uwezo wake wa kujieleza na uzoefu wake
wa ulimwengu wa kihalifu kumshawishi Suaréz na kumueleza kuhusu mkakati
wake wa kuiteka biashara ya mihadarati ya Cocaine nchini marekani na
akamdadavulia jinsi ambavyo yeye Suaréz atapata utajiri wa kupindukia
kama atakubali kufanya nae biashara.
Pia Pablo alimpa wazo Suaréz
kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini (Suaréz alikuwa
amefanikiwa kumpenyeza Mdogo wake serikalini na kuwa Waziri wa mambo ya
ndani) ahakikishe wanakutana na kiongozi wa Cuba Fidel Castro ili
wamuombe kuwa mshirika wao katika mambo kadhaa.
Suala hili
lilifanikiwa kwani Pablo na Suaréz walipata fursa adhimu na wakakutana
na Fidel Castro na ombi lao kubwa kwake lilikuwa ni kuwaruhusu kupitisha
mizigo yao nchini kwake Cuba na nchi za jirani pasipo bugudha. Pia
walimuomba aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanja vya ndege
vya Cuba na kujaza mafuta pale inapobidi kufanya hivyo.
Castro
akawakubalia kwa masharti mawili, moja ni kwamba atakuwa anawachaji
mamilioni ya dola za marekani kwa huduma hizo na pili mihadarati hiyo
isiuzwe ndani ya Amerika ya Kusini bali isafirishwe na kuuzwa Marekani
ambapo Fidel Castro alisisitiza kuwa atafurahi akiona vijana wa Mabepari
wakiharibika na mihadarati.
Masharti yote mawili haya
yakakubaliwa na Pablo na Suaréz kisha wakarejea Bolivia. Baada ya
kufanya mazungumzo juu ya namna watakavyo fanya biashara hatimae Pablo
na Suaréz walifikia muafaka na kwa mzigo wake wa kwanza alioununua
nchini Bolivia kutoka kwa Suaréz ulikuwa ni kilo 14 za unga gafi za
Cocaine.
Baada ya unga gafi kufikishwa nchini Colombia kwenye mji
wa Medellín, Pablo alikuwa ameandaa jengo maalum la ghorofa mbili
ambalo alilitengeneza kuwa maabara maalumu ambapo Cocaine gafi kutoka
Bolivia ilichanganywa na maligafi nyingine na kuboreshwa zaidi kikemia
na hatimaye kupata Cocaine daraja la kwanza aliyoihitaji tayari
kusafirishwa nchini Marekani kwa ‘walaji’.
Baada ya Cocaine
kutoka kwa Pablo kuingia kwenye soko la Marekani uhitaji na biashara ya
mihadarati ya Cocaine ilipaa kwa kasi ya ajabu na Pablo Escobar
akaanzisha rasmi genge lake la biashara ya mihadarati na akaliita
Medellíne Cartel.
Pablo akatengeneza mtandao madhubuti wa
wasambazaji wa mihadarati yake katika miji ya Florida na California
pamoja na majimbo mengine ya Marekani.
Pia akabuni njia mpya ya
kupitisha mihadarati kupitia Bahamasi katika kisiwa cha Norman’s Cay
takribani kilomita 350 kusini mashariki mwa pwani ya Florida.
Ili
kufanikisha zaidi azma yake Pablo Escobar alinunua nusu ya ardhi ya
kisiwa cha Norman’s Cay na nusu nyingine ikanunuliwa na swahiba wake wa
kimarekani aliyeitwa Robert Vesco ambaye pia alikuwa ndiye
anashughulikia masuala yake ya kibenki na uhasibu.
Katika Kisiwa
hiki Pablo alitengeneza uwanja wa ndege, bandari, hoteli, nyumba za
kuishi pamoja na ghala kubwa la jokofu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi
mizigo ya Cocaine kabla ya kuisafirisha kwenda marekani. Kwa kifupi hapa
ndipo kilikuwa kitovu cha kibiashara cha Genge lake la Medellíne
Cartel.
Pablo Escobar alikuwa amepania haswa kuliteka soko la
Cocaine Amerika ya Kaskazini na hii ilijidhihirisha kutokana na juhudi
zake alizozifanya kibiashara ili mda wote awe hatua kadhaa mbele tofauti
na washindani wenzake kibiashara.
Ili kufanikisha usafirishaji
wa mizigo yake kwa ufasaha na uhakika Pablo alinunua ndege za mizigo 15
za ukubwa wa kati na helikopta 6. Pia alinunua Nyambizi ndogo mbili
(submarines) kwa ajili ya kusafirisha mizigo mikubwa ya mihadarati.
Hadi kufikia mwaka 1985 Pablo alikuwa anasafirisha takribani tani 70
mpaka 80 za Cocaine kwa mwezi na alikuwa ameshikilia asilimia 80 (80%)
ya soko la mihadarati la Marekani.
Na katika kipindi hiki Genge lake
la Medellíne Cartel lilikuwa linaingiza kipato cha cha Dola Milioni 70
kwa siku (Shilingi Bilioni 140 za Kitanzania) na mapato yao kwa mwaka
mzima yalifikia Dola Bilioni 21.9. (Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania).
Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za
kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za
sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)
Ni katika kipindi hiki
ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu
namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika
historia ya Ulimwengu.
Kutokana na nguvu na ushawishi alionao,
Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la
Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha
Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).
Moja ya
majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za
kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka
1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini
Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika
nchi ya Uhispania.
****
Katika miaka ya 1990 utajiri wake
binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa
na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za
kitanzania)
Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la
Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi
ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.
Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali
kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of
Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia
(Colombia Liberal Party).
Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya
akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda
kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri
Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo
alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha
tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.
Sasa Endelea….,
Hacienda Nápoles: Pepo Juu ya Uso wa Dunia
Kutokana na utajiri uliopitiliza wa Pablo Escobar alithubutu
kutengeneza makazi ya kuishi ambayo namna pekee ya kuyaelezea ni kana
kwamba alijitengenezea ‘pepo’ akiwa duniani.
Katika mji mdogo wa
Puerto Triunfo, takribani kilomita 150 kutoka katika mji wa Medellín,
Pablo alinunua eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 20 na kujenga
makazi yake na familia yake na akayaita makazi haya Hacienda Nápoles
(Naples Estate).
Licha ya majengo ya kifahari ya kuishi yeye na
familia yake pia makazi haya yaliwekwa anasa lukuki zisizomothirika.
Ndani ya makazi haya kulikuwa na Uwanja wa ndege binafsi (private
airport), bustani maalumu ya sanamu za kuchonga na kufinyanga (Sculpture
Park), kulikuwa na sehemu maalumu ya kuhifadhi magari ya kifahari na
pikipiki za kifahari kwa ajili ya kutazama tu (collection), kulikuwa na
uwanja wa mbio za magari magogo (kart racing track), kulikuwa na uwanja
wa mapigano ya ng’ombe (Bullring), na pia ndani ya makazi haya kulikuwa
na mbuga ya wanyama ya kutengeneza (Zoo) ambapo Pablo alikusanya aina
mbali mbali za wanyama kutoka kila kona ya dunia na kuwaweka humo.
Katika geti la kuingia kwenye ‘pepo’ ya Pablo sehemu ya juu ya geti
ilininginizwa ndege (ndege halisi) kama urembo. Ndege hii aina ya Piper
PA-18 Super Cub yenye namba ya mkia HK-617-P hii ndio ilikuwa ndege ya
kwanza aliyoitumia Pablo kuingiza mzigo wake wa kwanza wa Cocaine nchini
Marekani.
Hapa katika ‘pepo’ hii ndipo ambapo Pablo Escobar aliishi yeye na familia yake.
Plata o Plomo
Moja ya vitu muhimu vya kihalifu alivyovifanya Pablo na kufanikiwa
kuibuka kama kinara wa uhalifu Amerika ya kusini ilikuwa ni kutekeleza
sera yake aliyoianzisha yeye mwenyewe ili kuidhibiti serikali na vyombo
vya ulinzi ambapo sera hii aliita “Plata o Plomo” (silver of lead (fedha
au risasi)). Akiwa na maana kwamba kama wewe ni mtu wa serikali na
ikitokea mmesigana basi atakupa fedha (rushwa) kama ukikataa kupokea
fedha basi anakupiga risasi.
Sera hii ilimfanya Pablo aogopwe na
watendaji wa serikali pamoja na vyombo vya usalama na ikapelekea wengi
kukubali ‘Plata’ (silver (fedha)) wakihofia kupoteza maisha endapo
wangekataa fedha kutoka kwa Pablo. Hii ilimsaidia Pablo Escobar kuwa na
vibaraka wengi katika serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.
Lakini sera hii iligharimu maisha ya watu wengi sana wale ambao
walikataa kupokea fedha kutoka kwa Pablo na mojawapo ya matukio mawili
yanayokumbukwa sana ya utekelezaji wa sera ya ‘Plata o Plomo’ ni haya:-
Mosi; Uvamizi wa Mahakama Kuu ya Colombia 1985.
Mwaka 1985 baada ya mabishano ya muda mrefu bungeni kuhusu vifungu vya
kikatiba vinavyokataza raia wa nchi ya Colombia kukabidhiwa kwa nchi ya
kigeni akiwa kama muhalifu hatimae serikali ikafungua kesi ya kikatiba
mahakama kuu ya Colombia ikitaka ruhusu ya kukabidhi baadhi ya wahalifu
kwa serikali ya Marekani ikitokea wakikamatwa.
Suala hili
lilikuwa linamlenga moja kwa moja Pablo Escobar kwani serikali ya
Colombia ilikuwa inapewa shinikizo kubwa na Marekani kuwa wafanye
marekebisho ya katiba ili iruhusu raia wa nchi hiyo ambaye ni muhalifu
kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni. Haya yalikuwa ni maandalizi endapo
ikitokea Pablo Escobar akikamatwa.
Pablo akajitahidi kwa juhudi
zake zote kuhonga serikalini na hata kutoa onyo kuwa mabadiliko hayo ya
kikatiba yasifanyike lakini serikali iliendelea na mchakato kutokana na
shinikizo walikuwa wanapata kutoka kwa marekani.
Inajulikana
kwamba Pablo mara kwa mara alikuwa akiapa mbele za watu wake wa karibu
kuwa kamwe hatokubali kufungwa katika nchi ya marekani na alikuwa na
msemo anaoupenda kuusema kwamba “ni heri kuwa kaburini Colombia kuliko
kuwa hai kwenye gereza la Marekani”.
Baada ya juhudi zake zote za
kuionya serikali kutobadili katiba kushindikana hatimaye Pablo akakodi
kikundi cha wapiganaji wa msituni kilichoitwa M-19 ili wasaidie kumaliza
tatizo lake.
Siku ya Novemba 6, 1985 majaji 25 wa mahakama kuu
walikuwa katika vikao vya mwisho kujadili na hatimae waweze kuridhia
mabadiliko hayo ya katiba lakini kabla ya kumaliza vikao vyao na
kuridhia mabadiliko hayo walivamiwa na wapiganaji wa kikundi cha M-19.
Wapiganaji hawa walivamia na kuteka mahakama kuu kwa muda wa siku mbili
na zaidi ya nusu ya majaji waliuwawa na waliosalia walichukuliwa
mateka.
Majaji hawa waliochukuliwa mateka walikuja kutumiaka kama
sharti muhimu la kuibana serikali waache kurekebisha katiba ili waweze
kuachiwa. Baada ya serikali kukubali kuacha kubadili katiba hasa
kipengele cha kukabidhi wahalifu kwa nchi ya kigeni, majaji wote
waliotekwa wakaachiwa.
Pili; Mauaji Mgombea Urais Luis Carlos Galán
Tukio la pili linalokumbukwa sana la utekelezaji wa sera ya ‘Plata o
Plomo’ lilikuwa ni mauaji ya mgombea Urais wa Colombia aliyeitwa Luis
Carlos Galán. Galán alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni nchi nzima na
alikuwa anatarajiwa kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa urais wa Colombia
wa mwaka 1990.
Moja ya sera kubwa aliyokuwa anaihubiri kila kona
ya nchi ilikuwa ni kupambaa na Magenge ya Mihadarati hasa hasa
akililenga Genge la Medellíne Cartel na kiongozi wake Pablo Escobar.
Pablo alimtumia barua kadhaa ambazo ziliwekwa nje ya nyumba yake kwenye
kisanduku cha barua akimuonya na kumtaka aachane na sera hiyo ya
kumsakama yeye pamoja na washirika wake wa Medellíne Cartel lakini Bwana
Galán alionekana dhahiri amezamilia kutekeleza sera hiyo endapo
angechaguliwa kuwa rais wa Colombia.
Akiwa katika kampeni Bwana
Galán alifanikiwa kufika kwenye mji wa Madellín ambapo Pablo alikuwa na
ushawishi mkubwa na wapo wananchi waliojaribu kumuua Galán kwa kumrushia
guruneti la kutupa kwa roketi (Rocket Propelled grenade) lakini kwa
bahati nzuri Bwana Galán akisalimika.
Baada ya hapo Pablo akakodi
wadunguaji maalumu kufatilia nyendo za Galán na akawapa amri ya kumpiga
risasi mara tu wakipata upenyo wa kufanya hivyo.
Wiki kadhaa
baadae akiwa kwenye kampeni katika mji wa Saocho Kiranga alipokwenda
kuhutubia wafuasi wake wapatao 10,000 waliokusanyika wakisubiri kumsikia
na mara baada ya kuwasili na kupanda jukwaani kuhutubia kabla hajatoa
hata salamu kwa wafuasi wake alidunguliwa na risasi na kupoteza maisha
papo hapo.
Tukio hili lilizua taharuki nchi nzima na imekuwa
skendali yenye utata mpaka leo hii nchini Colombia kwani kuna tetesi
kuwa viongozi wa serikali, polisi, pamoja na mashushushu walishirikiana
na Pablo Escobar kutekeleza mauaji haya.
Licha ya Pablo kuonekana
kama adui namba moja nchini marekani na baadhi wa watendaji wa serikali
ya Colombia hali ili kuwa tofauti kwa raia masikini wa Colombia ambao
wengi wao walimuona kama shujaa wao na katika mji aliozaliwa na kushi wa
Medellín anaonekana zaidi ya shujaa kwani mpaka leo hii wanamuona kama
ni aina fulani hivi ya masihi walipewa.
Hii inatokana na umahiri wa Pablo Escobar katika mahusiano na jamii iliyokuwa inamzunguka.
Pablo alikuwa ni mtu mwenye kusaidia masikini nchini Colombia pengine kuliko hata serikali yenyewe.
Pablo alijitolea kweli kweli katika kuboresha huduma za jamii kama vile
kujenga mahospitali, shule, nyumba za wazee, nyumba za kuishi kwa ajili
ya masikini na akawekeza fedha nyungi kujenga miundo mbinu ya Kanisa
Katoliki na nyumba za kuabudia. Pia Pablo alijenga vya kuendeleza watoto
katika mpira wa miguu, alifadhili klabu mbali mbali za wakubwa za mpira
wa miguu na alijenga viwanja vya kisasa kabisa vya mpira na michezo
mingine.
Ilifikia hatua mpaka Pablo alikuwa anawapa fedha taslimu wananchi wa Madellíne ili waweze kujikimu kimaisha.
Mambo haya yote yalifanya wananchi wampende na kufumbia macho uhalifu wote aliokuwa anaufanya.
Kwa mfano katika mji wa Madellín ilifikia hatua kana kwamba wananchi
wote walikuwa ni walinzi wake binafsi kwani walikuwa wakimtonya kila
walipoona polisi wageni wakiingia hata kwa siri kwenye mji huo. Au
wakati mwingine walikuwa wakitoa taarifa za uongo au kukataa kusema
chochote pindi wakiulizwa na vyombo vya ulinzi kuhusu nyendo za Pablo.
Hii ilimfanya Pablo azidi kujizatiti na kuongeza mahaba kwa wakazi wa Medellín na raia wa Colombia kwa ujumla.
VITA KUU YA KWANZA YA MAGENGE YA MIHADARATI.
Kuna msemo wanasema ‘adui wa adui yako ni rafiki yako’! Swali: je, inakuwaje pale adui wa adui yako akitishia maslahi yako??
Adui wa Adui yako (Kikao cha Kwanza)
Hapo baadae nitaeleza kwa kifupi kuhusu kuibuka kwa genge lingine
ambalo nalo lilishamiri katika biashara ya Cocaine lililoitwa Cali
Cartel hivyo kufanya kuwe na uwepo wa magenge mawili yanayoshindana
kibiashara yaani Medellín Cartel chini ya Pablo Escobar na Cali Cartel.
Licha ya ushindani wao wa kibiashara mwaka 1983 iliwabidi washirikiane
kwa sababu za msingi kabisa. kuliibuka kikundi cha wahuni waliokuwa
wanateka watu na kudai fedha kutoka kwa ndugu ili wawaachie. Baada ya
kuteka ndugu kadhaa wa viongozi wa serikali wahuni hawa wakaanza kuteka
ndugu wa mabosi wa Cartels na kudai pesa.
Moja ya watu muhimu
waliowateka alikuwa ni Marta Nieves Ochoa dada wa moja ya mabosi wa Cali
Cartel na watekaji walikuwa wanataka wapewe dila milioni 10 ili
wamuachie. Hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya mabosi wa Cali Cartel na
Medellín Cartel kukutana ili kuweka mkakati maalumu ambao utapeleka
ujumbe kwa wahuni na watekaji wote kuwa familia za mabosi wa Magenge ya
mihadarati ni mwiko kuzigusa.
Katika kikao hiki cha kwanza
Medellín Cartel na Cali Cartel waliunda kikosi kazi maalumu walichokiita
Muerte a Secuestradores (Death to kidnappers (Kifo kwa Watekaji)) au
kama kilivyojulikana kwa kifupi MAS.
Kila Genge lilichangia fedha, vifaa (silaha), na askari kwa ajili ya kikosi kazi cha MAS.
Kesho yake baada ya kikundi hiki kuundwa ndege ilipita juu ya uwanja wa
mpira wa miguu kuliko kuwa na mechi kubwa ikifanyika na kumwaga
vipeperushi kuhusu kutangaza zawadi nono kwa yeyeto atakayetoa taarifa
kuhusu kufahamu lolote juu ya wahuni wanaoteka watu na kushinikiza
wapewe hela. Jioni ya siku hiyo taarifa muhimu kutoka kwa wananchi
zikaanza kuletwa na kikosi kazi cha MAS mara moja kikaanza kukamata
wahuni wa vikundi vya utekaji na kuwatesa huku wakiwarekodi na kuwatumia
wenzao wanaoshikilia dada wa bosi wa Cali Cartel.
Ndani ya siku
tatu Marta Naives dada wa bosi wa Cali Cartel aliachiwa akiwa salama
salimini na huo ndio ukawa mwisho wa magenge ya wahuni kuteka
wanafamilia wa mabosi wa magenge ya mihadarati.
Kama ni rafiki yako, anaweza kuwa mshirika wako: Kikao cha Pili
Licha ya ushindani wa kibiashara kuendelea kuwepo kati ya Medellin
Cartel ya Pablo Escobar na Cali Cartel lakini kufanikiwa kwa mkakati wa
MAS kuliwapa moyo kuwa yako maeneo mengine mengi wanayoweza kufanya kwa
kushirikiana na yakawa na faida kwa pande zote mbili.
Sehemu ya
kwanza ambayo waliona inaweza kuwa na faida kwa pande zote mbili ilikuwa
ni Cali Cartel kukubali Pablo Escobar aweze kupitisha fedha zake haramu
katika benki ya First InterAmericans Bank ambayo ilikuwa inamilikiwa na
maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel. Hii ilikuwa na faida kwa kubwa kwa
Pablo kwani ilikuwa ni njia rahisi na salama kwake kuweza kusafisha
fedha zake haramu lakini pia ilikuwa na faida upande wa wamiliki wa
benki maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel kwani nao wangepata faida kwa
kutoa huduma hiyo kwa Pablo kutokana mabilioni ya dola ya dola ambayo
atakuwa anayapitisha kwenye benki yao.
Sehemu ya pili
waliyokubaliana kushirikiana ilikuwa ni namna ya kuratibu bei ya Cocaine
mtaani, kuratibu viwango vya ubora wa uzalishaji na njia salama za
kusafirisha mizigo.
Sehemu ya tatu walikubaliana kuhusu kugawana
soko. Cali Cartel wakakubaliwa kuendesha biashara kwenye jiji la New
York na Medellín Cartel ya Pablo Escobar wakapewa Florida na Miami. Jiji
la Los Angels likaachwa kama sehemu huru ambayo yeyote anaweza kufanya
biashara.
Kwa pamoja wakasonga na biashara ikashamiri.
Rafiki yako anapotishia maslahi yako: Vita Kuu ya Kwanza (Pablo Escobar VS Cali Cartel).
Biashara ya madawa ya kulevya katika America ya Kusini na duniani kote
kwa miaka yote imetawaliwa na vita kati ya magenge yanayopambana ili
kumiliki na kujipatia ushawishi zaidi katika soko. Lakini katika
historia hakuna vita ya magenge ya mihadarati iliyotisha na kuitikisa
Marekani na Amerika ya Kusini kama vita kati Medellín Cartel ya Pablo
Escobar dhidi ya Cali Cartel.
Vita hii ilitishia hata usalama wa uwepo wa Taifa la Colombia na kuleta aibu kubwa kwa serikali za Colombia na Marekani.
Lakini kabla sijaeleza chochote kuhusu vita hii, nieleze kwa ufupi tu kuhusu Cali Cartel.
The Cali Cartel
Cali Catel ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1970 kikiwa kama kikundi
maalumu cha wapiganaji kilichokuwa kinatumiwa na Pablo Escobar na
kilijulikana kama Las Chemas.
Moja wapo ya kazi walizozifanya kwa
mafanikio ilikuwa ni utekaji wa raia wawili wa nchi wa uswisi na
wakalipwa kiasi cha dola laki saba.
Baada ya malipo haya
washirika wa kikundi cha Las Chemas wakajitenga na Pablo Escobar na
kukimbilia kusini mwa nchi ya Colombia katika mji wa Cali na wakatumia
fedha hiyo kuanzisha biashara yao ya mihadarati na wakafahamika kama The
Cali Cartel.
Baada ya biashara yao kuanza kukua wakafanikiwa
kuwashawishi wanajeshi kadhaa waasi na kujiunga nao katika biashara na
wakafanikiwa kuwapata wengi.
Uwepo wa wanajeshi katika Cali
Cartel unadhihirishwa na mfumo wao wa kibiashara pamoja na uwezo wao wa
kufanya upelelezi na ushushushu (counterintelligence).
Kwa mfano
mfumo wao wa kibiashara ulikuwa tofauti na Medellín Cartel ya Pablo
Escobar ambayo yenyewe ilikuwa ni genge linalomilikiwa na mtu mmoja
(Pablo) ambapo Cali Cartel wenyewe walikuwa ni muunganiko wa
wafanyabiashara wanaojitegemea wanaounda genge/mtandao mmoja wa
mihadarati (Cali Cartel).
Kwa upande wa ushushushu na upelelezi
walikuwa mahili kiasi kwamba katika baadhi ya ripoti za CIA walikuwa
wanawaita kwa jina la utani “Cali the KGB”, wakiwafananisha na shirika
la upelelezi la Urusi ya kipindi hicho.
Turejee kwenye…’Vita Kuu’
Ushindani mkubwa wa kibiashara kati ya magenge haya mawili unaweza kuwa
sababu kubwa ya wao kuingia vitani lakini hii iliepushwa kutokana na
vikao vya makubaliano walivyokaa awalinkuhusu kugawana soko.
Sababu kubwa zaidi na ya msingi iliyochochea vita hii ilikuwa ni Pablo
kuamua kuacha kuheshimu makubaliano akiyoingia na Cali Cartel kutokana
na genge hili kujihusisha na vitendo ambavyo Pablo alivipinga kwa nguvu
zote.
Haijulikani ni kichaa gani kiliwapata viongozi wa ngazi za
juu wa Cali Cartel lakini ilipofika miaka ya kati kati ya 1980 Cali
Carteli wakaanza kujihusisha na imani zenye utata za “Kusafisha
Kizazi/jamii” (Social Cleansing). Cali Cartel walisimamia mauaji ya
mamia ya watu kwenye mji wa Cali pasipo sababu ya msingi wakidai kuwa
watu hao wanaichafua Cali.
Mauaji yao yaliwalenga walemavu,
machangudoa, watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, watoto wa
mitaani, na watu wasio kuwa na makazi.
Baada ya kuwaua
waliwaandika maandishi kifuania “Cali limpia, Cali linda” (Clean Cali,
beautiful Cali (Cali nadhifu, Cali inayopendeza)
Vitendo hivi
vilimkera Pablo na ikampa sababu ya kutokuheshimu makubaliano yake na
Cali Cartel kuhusu kugawana soko na akaamuru watu wake wafanye biashara
nchini marekani katika mji wowote ule wanaojisikia.
Kitu hiki
kikiwakera viongozi wa Cali Cartel na ili kumuonyesha kuwa wamechukizwa
wakaanza kutoa ufadhili kwa kikundi cha wapiganaji kilichokuwa kinajiita
Los Pepes amacho ni kifupi cha Los Perseguidos por Pablo Escobar
(People Persecuted by Pablo Escobar (watu walioumizwa na Pablo
Escobar)).
Kikundi hiki kilikuwa kinaundwa na ndugu za watu
waliouawa na Pablo au Wapambe wake na walikuwa wamejiapiza kumsaka na
kumuua Pablo popote alipo. Kitendo cha mabosi wa Cali Cartel kuanza
kukipa ufadhili kikundi hiki kilichochea moto wa vita ya magenge amabao
haukuwahi kuonekana hapo kabla.
Katika kipindi hiki Colombia
ilishuhudia mauaji ya kutisha ambapo wafuasi wa magenge yote mawili
walikuwa wakitafutana usiku na mchana. Mauaji haya yaliwahusu mpaka
marafiki, ndugu na wanafamilia wa makundi yote mawili. Katika mwaka 1988
pekee idadi ya vifo ilifikia zaidi ya watu 21,000 na mwaka 1989 idadi
iliongezeka mpaka vifo zaidi ya 28,000.
Hiki kilikuwa ni moja ya
vipindi vigumu zaidi kiusalama kwa Pablo kwani alikuwa na lundo la
maadui waliokuwa wakimtafuta. Kulikuwa na serikali ya marekani
inamtafuta, serikali ya Colombia inamtafuta, Kikundi cha Los Pepes
kinamtafuta, na genge la Cali Cartel linamtafuta. Kutokana na suala la
usalama kuwa tete mno ilimlazimu aame kutoka katika ‘pepo’ yake ya
Hacienda Napolés na kwenda kujificha katika nyumba za maficho juu ya
milima ya mji wa Madellín.
Ilikuwa inambidi abadili makazi mpaka
mara nne kwa siku moja. Nyumba zake nyingi hizi za juu ya milima alikuwa
anazitumia kuhifadhi pesa na silaha na ilitokea siku walienda kwenye
nyumba yake iliyopo karibia kabisa na kilele cha mlima na ilikuwa iko
ndani ya msitu mnene.
Siku hii kulikuwa na baridi lisilomithirika
na kutokana na nyumba hii kujengwa maalumu kwa ajili ya kuhifadhi fedha
na silaha haikuwa na mfumo wa joto wala umeme. Ilifikia kipindi cha
usiku baridi lilizidi na kupitiliza kiwangi cha kawaida mpaka ikaanza
kutishia afya ya mtoto wake wa kike aliyekuwa naye pamoja na familia
yake.
Kutokana na kutokuwepo na namna nyingine yeyote ya kupasha
moto nyumba hiyo ili kupunguza baridi, ili mbidi Pablo achome moto
maburungutu ya fedha usiku kucha ili kuipatia joto familia yake na hasa
mtoto wake wa kike ambaye alionekana kuathiriwa zaidi na baridi. Mpaka
asubuhi kunakucha na baridi kupungua kufikia kiwango cha kawaida Pablo
alikuwa ameteketeza maburungutu ya hela ya kiasi cha dola milioni mbili
za kimarekani.
Baada ya Juhudi za Cali Cartel kumpata Pablo
kutozaa matunda, walitoa kandarasi kwa Jorge Selcado ambaye alikuwa ni
muhandisi na Mwanajeshi. Jorge alikuwa maarufu kwa kuandaa timu maalumu
za mauaji ya kuratibiwa kiumakini (assassination teams) na mara zote
mipango yake inakuwa ya mafanikio.
Baada ya Jorge kupewa ‘ofa’
hii na mabosi wa Cali Cartel aliwasiliana na watu wake ambao walikuwa ni
wanajeshi wa kukodi (mercenaries) kutoka nchini uingereza ambao
walikuwa wamewahi kutumikia katika jeshi la Uingereza kitengo maalumu
cha Anga (SAS – Special Air Services).
Timu hii ilikuwa na watu
kumi mbili na iliwasili Colombia na kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa ili
kujiandaa na zoezi lililopo mbele yao. Walifahamu kuwa kwa kipindi
hicho Pablo alikuwa amejificha mahali kusiko julikana kwenye milima,
hivyo walisubiri wapate taarifa kuwa amerejea kwenye ‘pepo’ yake ya
Hacienda ili wafanye shambulio la kushitukiza.
Siku hiyo
haikuchelewa sana kwani timu ya Mpira ambayo Pablo alikuwa anaishabikia
na kuifadhili ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Colombia.
Hivyo Pablo alirejea jijini Medellín ili ajumuike kusherehekea ushindi
huo.
Kikosi hiki kilichotumwa kumuua Pablo walijiandaa na Chopa
mbili za kivita zilizobeba silaha nzito na mpango wao ulikuwa
wamshitukize Pablo nyakati za asubuhi na kufanya shambulizi nyumbani
kwake Hacienda Napolés.
Ili mpango huu uwe na ufanisi
walikubaliana kuwa washambulie kutokea nyuma ya milima na chopa ziruke
katika mfumo maalumu wa kijeshi wa usawa wa chini chini kabisa
(nap-to-earth) ili wasiweze kuonekana kutokea mbali.
Keshi yake
chopa ziliruka kuelekea Hacienda Napolés kama walivyopanga wapitie nyuma
ya milima huku zikiruka chini chini, lakini wakiwa kwenye milima hiyo
kwa bahati mbaya chopa moja ilimshinda rubani kutokana na kuruka chini
chini na ikagonga kwenye mlima na kudondoka.
Zoezi ambalo
kilipangwa kuwa la kwenda kushambulia na kumuua Pablo likageka kuwa ni
zoezi la uokoaji na mpango huu ukaishia hapo hapo.
Baada ya kufeli kwa zoezi hili serikali ya Colombia iliwasiliana na Pablo kujaribu kumuomba ajisalimishe.
Waliharibu kumbembeleza kwa kila namna ambayo waliweza na kumuahidi
watakubaliana na masharti yoyote atakayoyasema. Serikali ilifikia
kipindi walikuwa ‘desperate’ kutokana na aibu waliyokuwa wanaipata
kimataifa kwa kushindwa kumdhibiti muhalifu mmoja aliyeifanya nchi yao
ya Colombia mpaka kubatizwa jina la ‘Capital of death’ (mji wa kifo).
Hivyo matamanio yao ilikuwa tu kuutangazia ulimwengu kuwa wamemkamata
Pablo.
Baada ya Pablo kutafakari kwa kina na kuona jinsi usalama
wake na familia yake kuwa ni mdogo kutokana na maadui wanaomzunguka kila
kona akakubali ombi la serikali kujisalimisha lakini akawapa masharti
matatu.
Kila $1 aliyokua anaweka katika biashara yake alikua anapata profit OR return ya $200.
Alikuwa anakusanya pesa haweki bank, anatunza ndani chini ya ardhi, juu
ya dari or ukutani. Adui pekee wa hela zake walikuwa ni Panya wenye
njaa kali. Kila mwaka inasemekana alikua anapoteza 10% ya faida ambayo
kwa haraka haraka ni $b1, Panya walizokuwa wanakula.
Marekani na
Serikali ya Colombia ilitaka Pablo akamatwe na afungwe. Akakubali but
Gereza akajenga yeye. Ndani ya gereza kulikuwa ni kama 5star hôtel.
Alijiwekea kila kitu, Jacuzi, Bar, Pub, TV,na vitu kibao vya thamani.
Pia wanawake wakawa wanaingia na akiwa jela alikuwa ana uwezo wa kutoka
na kurudi kisirisiri, coz walinzi wa gereza alikuwa anawahonga vizuri
sana.
Baadae, Pablo alichoka maisha ya Jela la Hôtel, anataka
kurudi kitaa, akatoroka. Wakati anatoroka akachukua familia yake na
walinzi wake wakakimbilia Maporini. Wakati wapo huko vichakani, mtoto
akaugua ghafla na kukawa na baridi sana, ukahitajika moto unajua Pablo
alochofanya?
Alikuwa ananunua na kutumia Rubber band za $2,500 =
tsh 4,050,000 za kibongo kufungia hela zake kila mwezi, so kwa mwaka
alikuwa ananunua rubber band za $30,000 = 48,600,000 kufunga tu mihela
yake (hata BOT hawatumii rubber band za $2,500 kwa mwezi na haijawahi
kutokea kwa mtu wala taasisi)
Alinunua ndege kwa ajili ya
kusafirishia hela zake tu, kila trip ndege ilikuwa inabeba $10m. Mwaka
1989, Forbes ilimtaja kama tajiri wa 7 duniani, anakadiriwa kuwa na
utajiri wa $25-30b, watu wake wa karibu wanasema alikuwa anazidi hata
hapo coz kwa siku alikuwa anatengeneza sio chini ya $60m, coz kwa mwezi
alikuwa anasafirisha zaidi ya 80-100t USA.
Na ubabe wake wote,
Pablo alikuwa anaogopa sana kufa. Baada ya kutoroka Jela, serikali na
jeshi la Colombia wakawa wanamtafuta Pablo, akawa-offer serikali iachane
nae na atailipia serikali deni ililokuwa inadaiwa $b10 zaidi ya tirioni
18 za kibongo, ili serikali imalize deni inalodaiwa, lakini serikali
ilikataa, msako wa Pablo wakakabidhiwa wamarekani na kumuua December
2/1993.
Mpaka leo hongo/rushwa kubwa duniani kuwahi kutokea ni
hiyo ya $10b ya Pablo kutaka kulipa deni la taifa la Colombia, 10b usd =
trilioni 18.