Watu
wengi duniani hutumia mkono wa kulia kwa shughuli nyingi na si ajabu kwamba
vitu vingi huundwa kwa kuwafikiria wanaotumia mkono wa kulia.
Wanaotumia
mkono wa kushoto husumbuka sana katika kutumia vitu kama vile mkasi, vitabu au
hata kufungua milango.
Fikiria
pia kuhusu kipanya katika vituo vya kupokea huduma ya mtandao, mara nyingi
utapata kimewekwa upande wa kulia.
Kuna
pia viti vyenye sehemu ya kuandikia vyuoni, ni vichache sana hujengwa kwa
matumizi ya watu wanaotumia mkono wa kushoto.
Siku
ya watu wanaotumia mkono wa kushoto huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Agosti.
Siku
hii iliadhimishwa mara ya kwanza mwaka 1976.
Haya hapa ni baadhi ya mambo kumi ya kushangaza kuhusu watu
wanaotumia mkono wa kushoto:
1.Asilimia
kumi kati ya watu wote duniani hutumia mkono wa kushoto, na kiwango hiki
kimesalia hivyo kwa muda mrefu. Wanaume wana uwezekano mkubwa wa kuwa wanatumia
mkono wa kushoto.
2.Kwa
muda mrefu katika jamii nyingi, watu wenye kutumia mkono wa kushoto
walichukuliwa kuwa dhaifu. Si ajabu kwamba huenda uliwaona au unawaona watoto
wanaochapwa sana kwa kutumia mkono wa kushoto wakila au wakiandika. Katika
baadhi ya jamii, kutumia mkono wa kushoto huhusishwa na uchawi.
3.Kumsalimia
mtu kwa kutumia mkono wa kushoto kumekuwa kukitazamwa kama kumkosea mtu
heshima. Hii ni kwa sababu watu zamani walikuwa wakitumia mkono wa kushoto
kujitakasa baada ya kwenda msalani.
4.Bingwa
wa tenisi duniani Rafael Nadal alibadilisha na kuanza kutumia mkono wake wa
kushoto akicheza - kutokana na imani ya mkufunzi wake Toni Nadal kwamba
ingempatia nafuu kiasi akikabiliana na wachezaji wengine uwanjani.
5.Mrengo
wa kushoto? Jina hili lilianza kutumiwa miaka ya 1790 baada ya mapinduzi ya
Ufaransa na kuondolewa kwa utawala wa kifalme. Wawakilishi wa chama cha
kishoshialisto katika bunge walikuwa wakikaa upande wa kushoto wa kiongozi wa
vikao. Wat wa mrengo wa kushoto wakati huo walikuwa wakitazamwa kama maadui wa
wasomi na watawala.
6.Kwa
muda mrefu, dini ya Kikristo ilihusisha upande wa kushoto na maovu. Kwenye
picha nyingi za Siku ya Kiama, wale waovu (mbuzi) hutumwa upande wa kushoto nao
wale wa kuokolewa (kondoo) hutumwa upande wa kulia. Wakati wa kusulubiwa kwa
Yesu, mwizi aliyetubu alikuwa amewekwa upande wa kulia na yule mwovu alikuwa
upande wa kushoto.
7.Watano
kati ya marais wanane wa karibuni zaidi nchini Marekani hutumia mkono wa
kushoto kuandika. Marais hao ni Gerald Ford, Ronald Reagan, George H.W. Bush,
Bill Clinton, na Barack Obama.
8.Kuna
pahala penye jina Left Hand (Mkono wa Kushoto). Eneo hilo hupatikana katika
jimbo la West Virginia na hutokana na kijito cha Lefthand Run.
Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotumia au waliotumia mkono
wa kushoto:
- Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama
- Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
- Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
- Mwanamfalme William wa Uingereza
- Msanii Angelina Jolie
Sikio la kushoto
Kwa
jumla, watu 40% duniani hutumia zaidi sikio la kushoto kusikia, 30% hutumia
jicho la kushoto na 20% hutumia zaidi mguu wa kushoto.
Mabingwa wa tenisi
Ingawa
ni asilimia 10% ya watu duniani hutumia zaidi mkono wa kushoto, tangu kuanza
kwa enzi ya Open katika mchezi wa tenisi duniani, 23% ya mataji ya Wimbledon ya
mchezaji mmoja mmoja yameshindwa na wachezaji wanaotumia mikono ya kushoto.
0 comments:
Post a Comment