Saturday, August 12




Kuna “theories” nyingi na zote zinatoa majibu fulani lakini pia zinaacha nyufa ambazo zinasababisha kusiwe na jibu la kutosheleza kwa asilimia mia kuhusu mwanzo wa maisha. Katika uchambuzi huu nitaacha pembeni vitabu vya dini ambavyo pia vinaeleza mwanzo wa uhai kwa aina yake. Baadhi ya theories zinahusisha asili ya uhai kama ifuatavyo:

Kutoka kwenye Dunia iliyokuwa imeganda kwa barafu (Chilly start theory) 

Hawa wanasema barafu inawezakuwa ilifunika sehemu kubwa ya dunia na bahari zote miaka billion 3 iliyopita maana jua halikuwa linawaka sana kama ilivyo sasa. Sasa hizi "layer" kubwa sana za barafu zilitunza "organic compounds" katika sehemu yake ya ndani hivyo kuzikinga na uharibifu kutoka katika vurumai la anga lilokuwepo wakati huo. Pia baridi ilisaidia kutunza molecules hizi kukaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika na hivyo kupelekea maisha kuanza. Lakini ugumu unakuja pale kwenye nini hasa aina ya chagizo iliyopelekea maisha kuanza. Dhana hii imeelezewa zaidi hapa: Did life begin in ice?

Kutoka kwenye matundu ya volcano chini ya Bahari (Deep-sea vents theory)

Hii theory inasema inawezekana maisha yalianza kutokana na "hydrothermal vents" zilizoko chini ya bahari ambazo hutoa molecules zenye hydrogen nyingi sana. Sasa katika miamba yake inawekekana moleules hizi zilijazana sana na kusababisha aina fulani ya "reaction" iliyosababisha maisha kuanza. Hawa wanasansi wanaegemea kwenye ukweli kwamba hata leo hii enao lenye aina hii ya geothermal vents kuna nishati kubwa ya joto na kemikali na viumbe vingi sana vya baharini huendesha maisha kando kando na ndani ya yake. Ugumu unakuja ukitengeneza simulation katika maabara yenye hali sawa na zinazopendekezwa katika theory hii bado haileti matokeo yanayotarajiwa. Dhana hii imeelezewa zaidi hapa: Earth Life May Have Originated at Deep-Sea Vents
Kutokana na radi zenye chaji ya umeme (Electric spark theory)

Hii ya charge ya umeme ilileta changamoto sana maana chaji au cheche za umeme katika hali fulani za kimaabara zinaweza kutengeneza amino acids na sugars (hivi ni vyanzo vikuu vya maisha). Hali fulani za kimaabara ni mfano katika mazingira yaliyojazwa maji, methane, ammonia na hydrogen. Ilikuwa mwaka 1953 katika jaribio lililoonesha labda radi (kwa kuwa na electric charges) ilisaidia kutengeneza vyanzo vikuu vya maisha. Baada ya hapo ugumu kwa hii theory ukaja pale tafiti nyingi zilipoonesha katika hali ya Dunia ya zamani hakukuwa na hydrogen nyingi ya kuwezesha hii kitu ingawa inaonekana methane, ammonia na radi zilikuwa nyingi katika wakati huo. Dhana hii imeelezewa zaidi hapa: The Spark of Life | Astrobiology Magazine

Kutokana na msukumo wa udongo (Community clay)

Theory hii inapendekeza molecules za mwanzo za maisha zinaweza zikawa zimekutana katika udongo hii ni idea aliyoijenga mtaalam wa kemia wa Scotland, Alexander Graham Cairns-Smith katika chuo kikuu cha Glasgow. Anadai madini fulani na udongo yanaweza kuwa chanzo cha kujipanga kwa organic molecules kuwa aina fulani ya sehemu ya kiumbe na baadae molecules hizi kuanza kujipanga zenyewe. Dhana hii imeelezewa zaidi hapa: Life might have Evolved in Clay, Researchers Find : Biology : Nature World News

Ulimwengu wa asidi zenye protini (RNA world)

Deoxyribonucleic acid (DNA) zinahitaji protein ili ziform na protein zinahitaji DNA ili ziform. Hapo sasa ndio inakuja hii theory ya Ribonucleic acid (RNA) World ambayo inapendekeza kwamba kwa sababu RNA inatunza informations kama DNA na inafanya kazi ya catalyst kama protein yani inaweza kuapply pande zote basi ndio chanzo. Lakini ugumu unakuja sasa hizo RNA zilitokea wapi kwa mara ya kwanza. Ni ngumu sana kwamba ziliibukia tu alafu zikaanza kuji-replicate.Dhana hii imeelezewa zaidi hapa: The RNA World and the Origins of Life - Molecular Biology of the Cell - NCBI Bookshelf

Kutoka kwenye anga za mbali (Panspermia)

Hii ambayo inashikiliwa na wengi inasema maisha hayakuanzia hapa dunia bali yaliletwa na kimwondo kutoka anga za mbali. kwa mfano tunaweza kujionea vipande vya miamba na mawe vilivyotoka sehemu nyingine ambayo si duniani. hivyo theory hii inapendekeza vimwondo au kimwondo Fulani kilikuja na vijidudu(microbes) vilivyo sababisha maisha kuanza hivyo sisi wote asili yetu ni huko mbali angani. Sasa hapa ugumu unarudi kule kule kwamba sasa kama maisha hayakuanzia hapa duniani na huko angani yalikotokea yalianzaje? Dhana hii imeelezewa zaidi hapa: PANSPERMIA THEORY origin of life on Earth directed panspermia lithopanspermia meteorites - Panspermia Theory

Zipo na nyingine ila hii inatoa mwanga baadhi wanasayansi waonaje katika swala hili la mwanzo wa maisha. Jinsi maisha yalivyotokea ni kitendawili kimoja na jinsi maisha yalivyobadilika mpaka yalivyo sasa ni kitendawili kingine.

Maisha

Kuanza kwa maisha kwa maisha kama tuyajuayo inakadirwa kuwa 3,600 Ma au 3.6 Ga. (Ga =Billion Years ago). Matukio ya mwanzo ni kama kutokea kwa simple cells za kwanza prokarotes na hivyo hii ina maana kila kilichohai leo hii ikiwemo mimea na vijidudu vina chanzo kimoja. Baada ya hapo tukio la pili kubwa ni kuanza kwa photosythesis ambayo ndio ilileta oyxgen kama matokeo ya process hii.Hii inakadiriwa kuanza katika miaka bilioni 3.4 iliyopita (3.4 Ga.)


Tukio jingine kubwa ni seli ya kwanza yenye nucleous inayoitwa na wataalam uekarotes, hii ilitokea katika kipindi cha miaka bilioni mbili iliyopita (2 Ga.) . Baada ya kipindi kirefu  cha miaka bilioni moja yani (1 Ga) ndipo kiumbe mwenye seli nyingi alipo-evolve. Na baada ya hapa miaka nusu bilioni ilyofuatia ndipo kiumbe wa kwanza alipo-evolve.

Unaweza kuona kutoka kwenye uhai wa seli moja moja kama walivyo baadhi ya bacteria kuja kwenye seli nyingi kama walivyo viumbe wengine wadogo wanaishio majini ilichukua kipindi kirefu zaidi hata ya binadamu kuevolve kutoka kiumbe wa majini mwenye mapezi kama samaki.

Wanyama

Hawa tunaambiwa walitokea miaka milioni mia sita kabla ya sasa (600 Ma). Kuna kiumbe wa kwanza alafu baada ya muda  wa miaka milioni mia yani katika (500 Ma)  baadhi ya hawa viumbe wa kwanza wakaevolve kuwa samaki wa kwanza. Hapa kabla ya kuvunjilia mbali hii concept lazima kwanza tuuangalie muda huo unaotajwa kwa kweli ni mrefu sana. Hapa kuna mabadiliko kidogo kidogo yanayoweza kupelekea tofauti kubwa sana kama ikiangaliwa kwa ufupi.  Mfano dinosaurs wameishi duniani kwa kipindi cha miaka 165 milioni kabla ya kutoweka na sisi binadamu hatuna hata miaka milioni moja.

Mamalia

Kwanza tunaanza na mamalia ambaye sisi tupo kwenye group hilo. Mamalia nao tunaambiwa walitokea kwa katika kipindi fulani hawakuwepo. Katika miaka milioni mia mbili kabla ya sasa (200 Ma) anatokea mamalia wa kwanza jamii ya panya (rodent).  Kipindi hiki matukio yake zaidi ya hilo la kuanza jamii ya mamalia ni lile la dunia kuangukiwa na kimwondo kikubwa kilichofuta viumbe wengi sana wakiwemo wale jamii ya reptilia wakubwa (Dinosaurs) hii ni katika kipindi cha miaka milioni 90-110 iliyopita. Na tukio lingine ni ku-evolve kwa wanyama jamii ya sokwe katika kipindi cha miaka milioni 80 iliyopita.

Muda huu mrefu mamalia hawa waliishi kama jamii ya panya wengine juu ya miti kuwakwepa wale reptilia wakubwa na wadogo waliokuwa hatari sana. Kwa hiyo wataalamu hawa wanasema baada ya kimwondo kile kikubwa kilichofuta karibu asilimia 75% ya viumbe vyote duniani ndipo mamalia hawa waliosalimika walipata nafasi ya kuhama mazingira kitu kilichopelekea kuongezeka na baadhi ku-evolve.
(kutokana na vigezo hivi) 

Mtu kutoka jamii ya sokwe

Mtu anakadiriwa kubadilika au mabadiliko ya Mtu kutoka katika jamii ya sokwe yanakadiriwa kuanza kunako miaka milioni sita iliyopita (6 Ma). Ma = ”Million years ago” tutaitumia kuanzia hapa. Kabla ya kipindi hiki mwanadamu na sokwe wote walikuwa familia moja kwa maana ya wote walikuwa ni aina moja.  Matukio makubwa hapa ni zama za mawe miaka  milioni nne (4 Ma) kabla ya sasa mpaka miaka 3500 BC. Tukio lingine muhimu kwetu ni mwanzo wa aina ya mtu wa kale anayejulikana kama Homo genus katika kipindi cha miaka milioni mbili na nusu kabla ya sasa.

Katika kipindi hiki kirefu wale wataalam wa evolution wanatuambia ndipo Mtu alipitia mabadiliko mengi yanayomfanya kwa kiasi kikubwa awe jinsi alivyo leo hii hasa baada ya kuwa Homo genus kama nilivyoainisha katika hiyo paragraph hapo juu.



Watu walioishi mapangoni

Zama hizi zinarudi nyuma hadi miaka 400,000 BC. Kipindi hiki matukio makubwa yanayoweza kutajwa ni matumizi ya moto katika miaka ya kuanzia 125,000 BC na mwisho wa zama za barafu katika kipindi cha 110,000, hadi 10,000 BC. Katika kipindi chote hiki binadamu bado hana tofauti kubwa sana ya kimwili na alivyo sasa. Anatembea kwa miguu miwili na ana tofauti na jamii ya sokwe. Miaka hii yote hakuna cha maana sana kinachoweza kuchukuliwa katika kumbukumbu. Kwa hiyo Mtu ameishi kwa kipindi kirefu sana akiishi maisha ya aina moja yasiyokuwa na maendeleo mpaka pale alipogundua moto.

Watu walipoanza kuwa na lugha na utamaduni

Watu hawa wenye kuwasiliana kwa aina fulani ya lugha na wenye kufundisha vizazi vyao namna ya kuishi (utamaduni) walianza miaka 60,000 BC . Hawa ndio wanaanzisha zile zama za ”modern humans” kwa kuwa waliishi katika jamii ndogo ndogo na hawana tofauti kubwa na jinsi tulivyo sasa. Matukio makubwa katika kipindi hiki kirefu ni kuanzia pale mtu alipoweza kuhama sehemu moja mpaka nyingine na hasa kutoka bara la Africa kwenda maeneo mengine ya Dunia. Katika kipindi cha 50,000 BC Watu wanaanza kuwa na lugha fulani yani zaidi ya kelele au milio ya ajabu kama ya wanyama wengine jamii yao. Na kwa muda wa kati ya kipindi cha 40,000 BC hadi 15,000 BC, Mtu wa kwanza anahamia katika mabara mengine yenye majira ya baridi na changamoto tofauti.
Mwisho wa zama hizi ni katika kipindi cha 9000 BC pale walipoweza kupanda mazao fulani au kuanza kilimo. Baada ya zama hizi ndipo inafuata historia iliyorekodiwa.

0 comments:

-