Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli akiwa katika Gari maalum na kuwapungia
mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa sherehe za miaka
53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa
Jamhuri,[Picha na Ikulu.]26/04/2017
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania katika
Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo,ambapo Mgeni rasmi akiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli,[Picha na
Ikulu.] 26/04/2017
Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa
Tanzania JWTZ,pamoja na Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakiwa
katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya
Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo,Mgeni rasmi akiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli [Picha na
Ikulu.] 26/04/2017
…………………………………………………………….
Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April 2017,
ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini
Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kukagua
gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshma yake,
Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara
Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote
na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.
”Muungano ndio silaha yetu.
Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano kwa
nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye” amesema Rais Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli amewataka
watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio
chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais Magufuli amesema Tanzania
imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa
sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa
ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa
moja lenye nguvu.
Aidha amesema Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika
nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Rais ametaja mafanikio
mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na
kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha
miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli na nchi kavu.
Aidha Muungano umeimarisha na
kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka
kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.
Kwa mara ya kwanaza katika
historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za
Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni
ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha
Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali
yanakuwa Dodoma.
”Niwahahakikishie wana Dodoma
na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na
hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa
imehamia hapa” amesema Rais magufuli.
Sherehe za miaka 53 ya Muungano
zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa
viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama
Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa
Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi
wa chama na serikali.
Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano
mwaka huu ni ”Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige
vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii”
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017
0 comments:
Post a Comment