Wednesday, April 13

17 Sep 1976, Dar es Salaam, Tanzania --- Pres. Julius K. Nyerere of Tanzania at news conference at State House in Dar es Salaam. --- Image by © Bettmann/CORBIS

BINAFSI si muumini wa misaada kutoka nchi hizo zilizoendelea, naamini pia kuwa uhuru kamili ni kujitegemea ndani ya taifa. Kama wewe bado ni tegemezi basi jua bado haupo huru na hii ni kwa maisha binafsi ya mtu mmoja mmoja na hata kwa Taifa zima kwa ujumla.
Ukiangalia vizuri misaada ambayo Afrika inapokea ni midogo sana ukilinganisha na wizi wa hizi nchi kwa kutumia makampuni yao makubwa, kwa mfano makampuni ya madini hayajalipa ‘Corporate tax’ tangu yaanze kuchimba madini yetu hapa Tanzania.

Ni mwaka jana tu Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeingia makubaliano haya makampuni yaanze kulipa hata kiduchu tu, Nitoe mfano kidogo kwa mwaka wa jana kampuni ya ACCACIA zamani ikiitwa Barrick Gold iliuza dhahabu zenye dhamani ya dola bilioni 868 na hii ni figure wanayotupa wao, hatujui wametudanganya kwa kiasi gani, sasa tumia ‘exchange rate’ badili kwa shilingi ya Tanzania utaona mauzo hayo ni kiasi gani. Fikiri kisha chukua hatua.

Lakini wamekubali kulipa mwaka huu kwa mara ya kwanza dola milioni 20 ambayo italipwa kila robo ya mwaka dola milioni 5.

Hii kodi ukilinganisha na mauzo yao bila kujali gharama ni kiduchu sana na tena wamesema inaweza isilipwe vilevile kwa kuwa wanadai marejesho ya Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) hivyo inaweza ikatumika ku ‘offset’ tu. Sawa kuna mikataba ya akina Chief Mangungo huko hatuwezi kuendelea kuilea.
Unaweza kuona kwa hili tu jinsi ambavyo tunaliwa ‘either’ kwa wazee na viongozi wetu kuzembea katika mikataba walioingia ama kwa ujanja mkubwa wa hawa raia wa watoa misaada, vyovyote itavyokuwa ukweli ni kwamba tunaibiwa sana.

Nyerere alikataa kurithi mikataba walioingia wakoloni kwa niaba yetu hata kabla hajakabidhiwa nchi hii. Mwalimu Nyerere alimwambia malkia kuwa sitaihuisha mikataba yenu bila haya wala kuogopa kunyimwa uhuru.
Afrika hupoteza takribani dola bilioni 102 kila mwaka Na kati ya mwaka 1980 hadi 2009 tumepoteza dola trilioni 1.9 kwa sababu nilizozitaja hapo juu.
Na sisi tukiwemo, mwaka 2012 tulishtuka na tukarekebisha sheria zetu za madini lakini hizi kampuni zilizoingia mikataba kabla ya hii sheria haziitambui hii sheria kabisa na haiwahusu.
Haya mambo unaweza kuyafanya kwenye nchi iliyojaa watu wa aina yetu. Fananisha hizo fedha zinazopotea na vimisaada vya mamilioni wakati sie tunapoteza ma bilioni, ni kichaa tu atakaecha hii hali iendelee na mie wala siwalaumu wazungu sababu wao si malaika, wamewapata wajinga basi wamewapiga. Ni kama ambavyo watu wa mjini wanavyopenda kuwadanganya watu wa vijijini kwenye ununuzi wa maeneo na mazao.
China wamepanga kuipa Afrika dola bilioni 60 sasa hiki ni kiwango kidogo sana ukilinganisha na fedha tunazopoteza kila mwaka lakini viongozi wengi wa Afrika wanafurahia tu huu utumwa. Kesho akitaka kitu Mchina utamnyimaje sasa kwa mfano. Yaani misaada wanayotupa yote huwarudia na faida kubwa juu yake. Ni wakati sahihi tujitafakari jinsi tunavyoenenda.

Pamoja na kuwa tunaishi kwenye jumuiya ya kimataifa lazima tuwe na utimamu fulani na inapobidi tujitoe akili kidogo ili tuweze fanya mabadiliko makubwa. Huwezi wewe una madini mungu kakupa unaingia mkataba na kupuuza madini yako kama rasimali yako nikimaanisha mtaji wako unapoingia kwenye ubia na kutegemea kodi tu hii si sawa kabisa.

Hata wale waliorithishwa nyumba Kariakoo wametushinda kwasababu wakikuuzia kiwanja mikataba yao mingi huwa inawapa umiliki wa flow kadhaa kwenye jengo tarajiwa, sembuse wasomi wetu kwenye Madini yetu tunashindwaje kuwa na hisa zetu, Mbona kwenye gesi tunaweza kwa kiasi fulani.

0 comments:

-