Kiswahili ni Lugha ambayo inakuwa kwa kasi kilakukicha na kujizolea umaarufu duniani kote huku ikitengeneza fursa mbalimbali za maendeleo, kwa kuzingatia hayo Wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki (EALA) wamesema walimu wa masomo ya Kiswahili wasilalamikie ukosefu wa ajira badala yake wakatafute kazi katika nchi wanachama.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mbunge wa jumuhiya hiyo Shyrose Bhanji amesema uhitaji wa walimu wa Kiswahili katika nchi wanachama ni mkubwa hivyo walimu hawana budi kuchangamkia fursa hiyo.
“Watu waache kulalamikia ukosefu wa ajira kwani soko huria limepanua mipaka kwa nchi zetu hivyo wanaweza kutafuta ajira nchi wanachama na kunufaika na umoja huu”
Bhanji amesema watanzania hususani vijana wanayo nafasi kufanya biashara na kutafuta ajira katika nchi wanachama kama ilivyo kwa wanachama wa nchi nyingine wanavyotafuta ajira na kutafuta masoko nchini.
“Watanzania wasipojituma na kuchangamkia fursa hizo watabakia kuwa wasindikizaji na hawataona manufaa ya kuwa wanachama wa jumuiya hiyo”.
0 comments:
Post a Comment