Monday, April 11


Hamad-Rashid-620x311

NA RACHEL GABAGAMBI

Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. James Jesse amesema kitendo cha Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Dk. Shein kumteua Mwenyekiti wa Chama cha ADC Hamad Rashid kuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kinalenga kukizika Chama kikuu cha upinzani cha Wananchi (CUF).JAMES JESSE UDS

Akizungumza na mtembezi.com wakati akitolea ufafanuzi kuhusu viongozi watatu wa upinzani kupewa nafasi katika baraza la uwakilishi, Dk. Jesse amesema nafasi aliyoipata Hamad Rashid itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha chama chake cha ADC na kukididimiza Chama cha Wananchi (CUF).

Amesema hakuna kifungu cha sheria katika Katiba ya Zanzibar kinachomzuia Rais kumteuwa mtu yeyote hivyo anampongeza Dk. Shein kwa kuwateuwa wapinzani katika nafasi za uwaziri na ujumbe wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwa serikali itaimarika kwa kushirikiana na viongozi wenye sifa hata kama wanatoka upinzani.

Hivi karibuni Dk. Shein alifanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri na kumteuwa Hamad Rashid  kuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi huku Juma Ali Khatibu pamoja na Said Soud Said kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.

0 comments:

-