Pamoja na wawili kuvunja rekodi tofauti katika ulimwengu wa soka, lakini bado kuna rekodi kadhaa wawili hao bado hawajaweza kuzivunja – zikiwemo hizi 27 zinazohusiana na michuano ya klabu bingwa ya ulaya.
Messi na Ronaldo, ndio top scorers katika michuano hii huku Messi akiwa na magoli 80 na Ronaldo 89, lakini rekodi zifuatazo bado wafalme hawa wawili wa soka la kizazi hiki bado hawajafanikiwa kuzivunja:
1—Rekodi ya magoli mengi katika fainali za ulaya: Magoli 7, Alfredo Di Stefano, Ferenc Puskas, wachezaji wa zamani wa Real Madrid ndio wanaishikilia rekodi hii ya kufunga magoli katika fainali za michuano ya ulaya.
2—Kufunga katika fainali nyingi za michuano ya ulaya (Fainali 5): Kwa mara nyingine tena gwiji wa soka wa Madrid Alfred Di Stefano ndio mchezaji ambaye amefunga kwenye fainali nyingi za michuano ya ulaya mwaka 1956, 1957, 1958, 1959, na 1960.
3—Kufunga Magoli katika fainali moja ya michuano ya ulaya/Europa League: Rekodi hii inashikiliwa na gwiji wa Real Madrid Puskas ambaye alifunga magoli manne mnamo mwaka 1960.
4—Kufunga magoli mengi katika fainali ya Champions League final: Magoli 2, Massaro kutoka AC Milan 1994], Riedle [Dortmund, 1997], Crespo [Milan, 2005], Inzaghi [Milan, 2007], Milito [Inter, 2010]).
Messi na Ronaldo wameshafunga katika fainali mbili za UCL, kila mmoja akifunga goli moja katika fainali mbili tofauti. Messi aliifunga Man United mnamo mwaka 2009 na 2011, wakati Ronaldo amefunga mwaka 2008 akiwa na Man UTD na 2014 akiwa na Real Madrid.
5—Kufunga magoli mengi katika hatua ya makundi ya Champions League: Raul Gonzalez ndio anayeshikilia hii rekodi akiwa amefunga magoli 53. Messi amefunga 47 na Ronaldo amefunga 49.
6—Kufunga magoli mengi katika hatua ya robo fainali ya European Cup/Champions League: Di Stefano amefunga magoli (14).
7—Magoli mengi katika nusu fainali ya European Cup/Champions League: Di Stefano amefunga magoli (11) katika hatua hii.
8—Kushinda fainali nyingi zaidi na timu tofauti: Clarence Seedorf ameshinda fainali 3 na timu tofauti (Ajax 95, Madrid 98, Milan 03 na 07). Ronaldo ameshinda fainali 2 (Man Utd na Real Madrid) Wakati Messi ameshinda na UCL akiwa na klabu moja tu FC Barcelona.
9—Kuzifungia timu nyingi katika Champions League: Timu 6, Zlatan Ibrahimovic amevifungia vilabu sita tofauti katika michuano ya ulaya – Ajax, Juventus, Inter, Barcelona, Milan, PSG.
Messi ameifungia FC Barcelona tu katika maisha yake, wakati Ronaldo ameshaifungia Manchester United na Real Madrid.
10—Mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi katika fainali ya Champions League final: Paolo Maldini ndio mwenye rekodi hii, alifunga goli kwenye fainali ya UCL akiwa na miaka 36 na siku 333 vs. Liverpool, mnamo mwaka 2005.
11—Mfungaji mwenye umri mkubwa katika hatua ya makundi: Francesco Totti ndio mwenye rekodi hii, alifunga goli akiwa na miaka 38 na siku 59 vs. CSKA, 2014.
12—Mfungaji mwenye umri mkubwa katika fainali ya European Cup: Manfred Burgsmuller alifunga akiwa na miaka 38 na 293 katika mechi kati ya Werder Bremen-Dynamo Berlin, 1988.
Ronaldo hatoweza kuzivunja rekodi hizi za ufungaji 3 za juu mpaka mwishoni mwa msimu wa 2021-22, wakati Messi itambidi asubiri mpaka msimu wa 2023-24 (ikiwa timu zao zitafika fainali ya ulaya).
13—Goli la haraka zaidi katika Champions League: Roy Makaay anashikilia rekodi hii, alifunga goli mapema zaidi, sekunde ya 10.12 katika mechi kati ya Bayern Munich-Real Madrid, 2007.
14—Goli la haraka zaidi katika fainali ya Champions League: Paolo Maldini alifunga goli la mapema zaidi katika fainali ya UCL (53 seconds) Milan-Liverpool, 2005.
15—Hat trick ya haraka zaidi katika Champions League: Bafetimbi Gomis (8 minutes), 2011.
16—Kufunga hat trick mara mbili mfululizo: Luiz Adriano anashikilia rekodi hii, alifunga hat trick mara mbili mfululizo vs. BATE na BATE.
Messi na Ronaldo wana rekodi ya kufunga hat tricks nyingi zaidi katika michuano ya ulaya – kila mmoja akifunga mara 5, ingawa hawajaweza kufunga hat tricks za haraka zaidi – hat trick ya Messi ya haraka zaidi ni dakika 22 vs Arsenal na Ronaldo hat trick yake ya haraka zaidi ni dhidi ya Malmo msimu huu – dakika 12.
17—Kufunga katika misimu 14 mfululizo ya Champions League: Rekodi hii anaishikilia Raul
18—Kufunga magoli katika misimu mingi zaidi ya Champions League: Ryan Giggs ndio anaongoza kwenye rekodi hii, amefunga katika misimu 16 ya michuano hii.
19—Kufunga magoli mengi katika msimu mmoja wa michuano ya ulaya: Radamel Falcao ndio mwenye kuibebea rekodi hii, alifunga magoli 18 katika msimu mmoja akiwa Porto.
20—Kufunga katika mechi nyingi mfululizo: Ruud van Nisterlrooy alifunga katika mechi 9 mfululizo akiwa na Manchester United – msimu wa 2002-03.
0 comments:
Post a Comment