Bi Congcong alisomea shule ya wasichana ya Feza
Msichana kutoka
China ameibuka wa pili kwa ubora katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa
kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).
Congcong Wang, 16, alifanyia mtihani wake shule ya upili ya wasichana ya Feza iliyoko eneo la Kinondoni, Dar es Salaam.Ameambia wanahabari kwamba ameshangazwa sana na matokeo hayo.
"Sijawahi kudhani ningekuwa mmoja wa wanaoongoza. Nimekuwa nikitia bidii masomoni lakini sikutarajia hili,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen.
Alijiunga na shule za Feza mwaka 2006 akitokea China na akalazimika kujifunza Kiswahili na Kiingereza.
Jumla ya wanafunzi 240,996 walifanya mtihani huo wa kitaifa Novemba mwaka jana.
RSS Feed
Twitter
February 20, 2016
Unknown
0 comments:
Post a Comment