10:37 Kiongozi
wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo asema kwa maoni ya kundi lake la
waangalizi, uchaguzi ulitimiza viwango vinavyohitajika kimataifa.
Ahimiza walioshiriki kukubali matokeo. Awataka wasioridhika kutumia
mifumo ya sheria kulalamika. 10:30 Kiongozi wa
waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo anasema kulikuwa na changamoto katika
kuandaa vituokwa upigaji kura pamoja na kufunguliwa kwa vituo. Asema pia
waliona mabango ya kampeni katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.
Asema siku ya uchaguzi, baadhi ya wapiga kura walikosa majina yao
vituoni. Wasiojua kusoma hawakusaidia vyema. Waliofaa kupaka watu wino
baada ya kupiga kura katika baadhi ya maeneo hawakumakinika sana.
Apendekeza vifaa vya kupigia kura viwe vikifikishwa mkesha wa siku ya
kupiga kura, sawa na kuandaliwa kwa vituo. 10:25 Kiongozi
wa waangalizi wa COMESA Ashraf Gamaal Rashed amesema Tume ya Uchaguzi
inafaa kuwezeshwa zaidi ili kutekeleza majukumu yake vyema. 10:20 Waangalizi
wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA na IGAD wanatoa
taarifa zao kuhusu uchaguzi. Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan
Mwinyi amewapongeza wananchi wa Uganda kwa kujitokeza kwa wingi. Amesema
uchaguzi ulifiofanyika wiki hii ulikuwa na ushindani mkubwa.
09:59 Ubalozi
wa Marekani nchini Uganda umekanusha taarifa ambazo zimekuwa
zikisambazwa mitandaoni zikiashiria kwamba Marekani imewaagiza raia wake
waondoke Uganda. Ubalozi huo umesema taarifa hizo ni za uongo. 08:44 Bw
Kiggundu amesema matokeo mengine yanatarajiwa mwendo wa saa nne, lakini
yanaweza yakatangazwa mapema iwapo yatakuwa tayari. Ametetea tume hiyo
dhidi ya madai kwamba kura kutoka 'ngome za upinzani' hayajaripotiwa.
Tume inatarajiwa kutangaza matokeo kamili kabla ya saa kumi alasiri kwa
mujibu wa sheria.
08:38 Matokeo yaliyotangazwa sasa
hivi ni kama ifuatavyo. Ni kutoka vituo 21,254 kutoka kwa vituo 28,010.
Matokeo yaliyotangazwa yanajumuisha kura 7,822,737 ambazo ni sawa na
asilimia 51,21 ya wapiga kura 15 milioni waliosajiliwa na tume hiyo.
Kumbuka si wapiga kura wote waliosajiliwa ambao hufanikiwa kupiga kura.
Matokeo kwa sasa (Vituo 21,254 kati ya 28,010)
Abed Bwanika
70,708
0.95%
Amama Mbabazi
112,071
1.50%
Baryamureeba Venasius
42,931
0.58%
Benon Biraaro
20,553
0.28%
Kizza Besigye
2,603,880
34.94%
Joseph Mabirizi
19,661
0.26%
Maureen Kyalya
32,773
0.44%
Yoweri Museveni
4,549,148
61.05%
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
08:33 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu anaanza kutangaza matokeo ya karibuni zaidi. 08:32 Kwa sasa ni wakati wa maombi Namboole, kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza ya urais ya karibuni zaidi leo. 08:28 Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM Justine Kasule Lumumba amekuwa akiwahutubia wanahabari kutoka Bweyogerere
Museveni
anaongoza. NRM inaongoza katika kura za urais na za ubunge na
tunasubiri matokeo ya mwisho. Hata kule mawaziri wameshindwa, ni watu wa
kawaida. Waganda waliamua nani anafaa kuwaongoza. Kwa NRM si habari
njema, lakini ni lazima tukubali. 08:13 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuhutubia wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda saa sita kasorobo. 08:10 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu ameingia ukumbini kutangaza matokeo ya karibuni zaidi ya uchaguzi. 07:54 Tume ya taifa ya uchaguzi Uganda inatarajiwa kutoa matokeo mengine mwendo wa saa mbili asubuhi. 07: 52 Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa ni kama ifuatavyo:
Matokeo kwa sasa (Vituo 15,799 kati ya 28,010)
Abed Bwanika
51,150
Amama Mbabazi
88,900
Baryamureeba Venasius
33,135
Benon Biraaro
15,588
Kizza Besigye
1,767,041
Joseph Mabirizi
14,757
Maureen Kyalya
24,536
Yoweri Museveni
3,156,070
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
07:50 (Saa za
Afrika Mashariki) Hujambo! Twatumai umeamka salama. Karibu kwa taarifa
za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda. Matokeo ya uchaguzi wa
urais uliofanyika Alhamisi nchini Uganda yanaendelea kutangazwa, matokeo
kamili yakitarajiwa kutolewa baadaye leo alasiri.
0 comments:
Post a Comment