NI lazima uwe na watu ambao unataka kuwa
kama wao. Hayo ndiyo maisha. Kujua njia walizopitia hadi kufika mahali
unapopatamani ni moja ya ngazi muhimu sana kukusogeza katika maisha
hayo.
Kassim Kayira, kama anavyojulikana
katika ulimwengu wa habari kuwa ni miongoni mwa waandishi nguli kabisa
wa kimataifa, anasimulia safari yake ya maisha tangu kuzaliwa hadi
kufikia mafanikio aliyonayo katika habari.
Hii ni sehemu ya tano, akisimulia hatua
kwa hatua. Wiki iliyopita, tuliishia pale wakati wa mazungumzo yakiwa
yamekolea, ghafla namuona Kayira akiinuka na kuniambia jambo ambalo
linanifanya nikose raha ghafla.Je, ni lipi hilo?
SHUKA NAYO SASA…
SHUKA NAYO SASA…
“Aise, hebu ngoja kwanza nimuone bosi
huko ofisini, maana wakati ule alikuwa na wageni lakini alinitaka niwe
namuangalia mara kwa mara, sidhani kama leo tutamalizia mahojiano haya
na kama nilivyokueleza, kuwa kesho natakiwa kusafiri kwenda nchini
Uganda, ngoja tuone,” anasema Kayira akiwa ameshikilia kitasa cha mlango
cha chumba hicho, tayari kwa kuondoka huku akinitaka nimsubiri.
“Oke, hakuna shida,” namjibu kwa sauti ya unyonge.
Hata hivyo, dakika tatu au nne baadaye, ghafla mlango wa chumba hicho unafunguliwa na Kassim anaingia kwa kasi kama aliyekuwa akifukuzwa.
Hata hivyo, dakika tatu au nne baadaye, ghafla mlango wa chumba hicho unafunguliwa na Kassim anaingia kwa kasi kama aliyekuwa akifukuzwa.
“Sasa, inabidi twende kule Tazara kuna
mzigo nataka nikachukue huko, lakini mazungumzo yaendelee ndani ya gari,
tayari nimeshapewa dereva wa kunipeleka,” anasema Kayira na kulivaa
vyema begi lake mgongoni, tunatoka nje na kupanda gari maalum lililokuwa
na nembo nyingi za Azam TV.
“Mmmh, ikawaje kaka?,” naamuuliza ili aendelee na simulizi yake.
“Basi bwana, kazi ikazidi kunoga, nikiwa bosi mkubwa kabisa pale TV Rwanda, lakini sikuridhika na hapo kabisa, nikazidi kuwa mbunifu, lakini wakati hayo yakiendelea, umaarufu nao ukashika kasi,” anasema Kayira na kuachia tabasamu la kiaina.
“Basi bwana, kazi ikazidi kunoga, nikiwa bosi mkubwa kabisa pale TV Rwanda, lakini sikuridhika na hapo kabisa, nikazidi kuwa mbunifu, lakini wakati hayo yakiendelea, umaarufu nao ukashika kasi,” anasema Kayira na kuachia tabasamu la kiaina.
“Mwaka 1998, nilienda nchini Zambia kwa
masomo maalum katika Chuo cha Thomson Foundation, ambako nilisoma
Kiingereza na Kozi ya Utawala katika Utangazaji (Broadcasting
Management).
“Baada ya hapo, nikafanya kazi kidogo,
lakini nikaenda nchini Uingereza katika Chuo Kikuu cha Wales kuchukua
masomo ya juu na niliporudi nchini Rwanda, tayari nikawa mhariri mkuu wa
habari katika Televisheni ya taifa,” anasema Kayira.
“Lakini du, hapa acha niseme jambo moja,
wanawake wa Rwanda wana majaribu sana aisee, unajua duniani kote,
hakuna wanawake wazuri kwa maana ya maumbo kama Wanyarwanda,
kilichonisaidia ni kuwa tayari nilikuwa nimeshaoa na pia mimi ni mtu wa
dini sana.
“Lakini aaah, yalikuwa ni majaribu
makubwa, maana nilikuwa katika kiwango changu cha juu cha umaarufu, aah,
Rwanda, wewe acha tu ni kwa vile maisha hayawezi kurudisha siku za
nyuma,” anasema Kayira.
“Kufikia hapo, nikateuliwa kuwa natembea
na rais kwenye ziara zake, kwa kweli nilizunguka sana na Rais Kagame,
nimetembea nchi nyingi nikiwa na rais kama mwandishi wa habari wa
Televisheni ya taifa,” anasema Kayira.
“Nini umejifunza na kufaidika katika
ziara za rais?” namuuliza lakini badala ya kujibu swali langu, Kayira
anaingiza kitu cha tofauti kidogo.
“Unajua nafurahia sana uwepo wako na mimi kwa leo,” anasema kwa Kiswahili chenye lafudhi ya Kiganda.
“Kwa nini?” namuuliza na kumtazama usoni.
“Mimi nimefanya mahojiano na watu wengi sana duniani, lakini pia nimefanyiwa mahojiano na waandishi kadhaa, lakini naona una kitu cha ziada,” anasema Kayira na kutabasamu.
“Mimi nimefanya mahojiano na watu wengi sana duniani, lakini pia nimefanyiwa mahojiano na waandishi kadhaa, lakini naona una kitu cha ziada,” anasema Kayira na kutabasamu.
“Mmh, hebu jibu swali langu la awali,” naishia.
“Oke, faida ni nyingi sana, marupurupu mengi, kujua maisha binafsi ya rais na mambo mengine mengi zaidi,” anasema Kayira.
“Kujua maisha binafsi ya rais, kivipi?” namuuliza kwa shauku ya kutaka kujua maana halisi ya sentensi hiyo.
“Oke, faida ni nyingi sana, marupurupu mengi, kujua maisha binafsi ya rais na mambo mengine mengi zaidi,” anasema Kayira.
“Kujua maisha binafsi ya rais, kivipi?” namuuliza kwa shauku ya kutaka kujua maana halisi ya sentensi hiyo.
“Aaah, unajua rais anapokuwa ziarani,
anakuwa yeye kama yeye, japo nafasi na hadhi yake kama rais viko
palepale lakini yanakuwa ni maisha ya kibinafsi zaidi,” anasema Kayira.
“Sijaelewa, fafanua zaidi kaka,” namuuliza tena, safari hii naacha kuandika ili nimsikilize kwa makini zaidi.
“Yaani rais anakuwa akijiachia zaidi kwa
maisha binafsi, mnakuwa na mazungumzo ya kawaida na rais kama washkaji,
mnakula pamoja, mnataniana kidogo, yaani mnapata nafasi ya kumjua rais
zaidi ya nafasi aliyonayo,” anajitahidi kufafanua Kayira.
ELIMU
“Sawa, nimekuelewa sasa, nitakupigia
tena badaye, niko na mazungumzo muhimu hapa,” anasema Kayira kupitia
simu, akimpa maelekezo mtu aliyekuwa akizungumza naye.
“Basi, kwa hiyo mimi nilianza kusoma
mwaka 1979 katika Shule ya Msingi Mbarara, lakini sikufika hata darasa
la pili, kutokana na vita iliyokuwa ikiendelea kati ya Uganda na
Tanzania, kwenye harakati za kumuondoa Dikteta Nduli Idd Amin Dadaa,
sikuweza tena kuendelea na masomo,” anasema Kayira na kunitazama sana
usoni bila kupepesa macho.
“Mmh, ikawaje sasa?,” nami najikuta nikimtupia swali bila kujali jinsi alivyokuwa akinikazia macho.
“Dah! Nakumbuka mbali sana Brighton,
historia ya maisha yangu huwa siisimulii mara kwa mara, inauma sana,”
anasema Kayira na kuendelea;
“Wazazi wangu walilazimika kuhamia
nchini Rwanda, ingawa ni nyumbani kwao na mama kama nilivyokwishaeleza
kuwa ni Mnyarwanda, lakini tuliishi kama wakimbizi, hapakuwa na furaha
niliyoizoea Uganda,” anasema Kayira.
Kayira anasema, maisha yalibadilika sana
kwani baadhi ya jamii waliwaona ni wakimbizi, licha ya mama yao kuwa
raia wa nchi hiyo, anasema kilikuwa kipindi kigumu mno. Alipotezana na
baadhi ya rafiki zake kutoka nchini Uganda, kuna waliouawa kwenye vita
na kuna waliokimbilia sehemu mbalimbali kunusuru maisha yao.
“Zilikuwa ni siku mbaya sana,
tukalazimika kuishi kwenye kambi ya wakimbizi japo ilikuwa ni kwa siku
chache mno kabla ya kupata sehemu nzuri, namshukuru sana Mungu kwa
kuninusuru na janga hilo la vita,” anasema Kayira lakini hapohapo,
namuona akiinuka kidogo na kutumbukiza mkono wake wa kuume kwenye begi
dogo lililokuwa mapajani kwake, anachomoa kitu kama karatasi yenye
michoro na maelezo kadhaa.
Bila kusema chochote, ananisogelea na kuanza kuikunjua karatasi hiyo huku akichukua kalamu yake iliyokuwa kwenye mfuko wa shati.
“Hii ndiyo ramani ya Mbarara nchini
Uganda nilikozaliwa na kuanza kusoma kabla ya kukimbia kwa sababu ya
vita,” anasema Kayira huku akinionesha kwa kutumia kalamu hiyo.
“Ok,” najibu kwa sauti ya chini na kuendelea kuitazama ramani hiyo.
“Kwa hiyo nikapelekwa tena shule, ujue
baba yangu ni mtu anayependa sana elimu, ya dunia na haswa ya dini, kama
nilivyokueleza anaitwa Alhaji Ibrahim Kayira, huyu ni Sheikh, kwa hiyo
ni kwa namna gani unaweza kuona vile baba alikuwa amekolea kwenye mambo
ya dini,” anasema Kayira kwa lafudhi ya Kiganda na kwa msisitizo zaidi.
“Nikaanza kusoma tena kwenye Shule ya
Msingi Rwanda Islamic Center au Rwandan Centre Islamique kwa Kifaransa,
lakini hata mwaka haukuisha, na mwaka 1980 tukarejea tena nchini Uganda
baada ya hali kutulia, ilikuwa ni balaa tupu,” anasema Kayira.
“Kwa hiyo nikaendelea tena kusoma Shule
ya Msingi Mbarara hadi mwaka 1983, nikahamishiwa tena nchini Kenya na
kujiunga na Shule ya Msingi Machaakos Township hadi mwaka 1987.
AREJEA TENA UGANDA KWA MASOMO YA CHUO
“Nilipohitimu masomo ya msingi nchini
Kenya, nilirejea tena nyumbani Uganda na kujiunga na shule ya sekondari
iliyokuwa chini ya Taasisi ya Kiislamu (Bilal Islamic Institute), ambapo
nilisoma kidato cha kwanza hadi cha sita, kuanzia mwaka huo wa 1987
hadi 1992,” anasema Kayira na kukohoa kidogo.
“Nilipohitimu masomo ya sekondari,
nilifaulu vizuri, lakini nikawa nahisi kama naweza kuwa mwalimu, hivyo
nikaamua kusomea ualimu na kuchukua shahada ya elimu,” anasema Kayira.
Je, nini kitafuata? Usikose kufuatilia wiki ijayo kwa muendelezo wa simulizi hii tamu ya gwiji huyu katika tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment