Wednesday, February 17


Rio-Ronaldo
Rio Ferdinand amemjibu Cristiano Ronaldo baada ya kudai kuwa wakati wa kinyang’anyiro cha kuwania na hatimaye kuchukua UEFA mwaka 2008 hakuwa akiongea na mchezaji yeyote wa timu hiyo pindi alipokuwa nje ya uwanja.
Kuelekea mchezo wao wa UEFA leo usiku dhidi ya Roma, Ronaldo amesema kuwa anafananisha mahusiano yake na ‘utatu’ wa Madrid kama wakati alipokuwa akicheza Manchester United.
Hayo yamekuja baada ya Ronaldo kuulizwa kuwa, haoni utatu wa Barcelona (Messi, Neymar na Suarez) unafanikiwa kwa sababu ya ukaribu baina yao ilhali mambo yakiwa tofauti kwa upande wa Madrid.
“Wakati nikiwa Manchester United nilishinda ligi ya Mabingwa na sikuwa nikiongea na Rio Ferdinand, Ryan Giggs au Paul Scholes. Tulikuwa tukisamiliana tu baada ya hapo kila mtu akaendelea na mambo yake.”
Rio-Ronaldo 1
Baada ya kauli hiyo, Ferdinand aliulizwa juu ya uhusuano wake na mchezaji huyo wa zamani wa United baada ya mchezo wa PSG na Chelsea na ndipo akajibu:
“Sidhani kama anachoongea ni sahihi!” alisema beki na nahodha huyo wa zamani wa United.
“Mlango wa chumba chake na changu ilikuwa ikiangaliana. Siamini kabisa aisee.”
Tuhuma hizo zimekuja baada ya Ronaldo kusema:
“Tukiwa uwanjani tunapambana kwa sababu ya mafanikio ya timu
“Kukumbatiana na kubusiana hakuongezi chochote.
“Sio jambo la msingi kwa Bale kuja kwangu kula chakula cha usiku au mimi niende kwake nikale. Sisi sote ni weledi bana.

0 comments:

-