Thursday, January 14


Maeneo hayo ni pamoja na eneo maarufu kwenye ufuo wa bahari la Marine Drive na ufukwe wa Girgaum Chowpatty ambayo yote ni kivutio cha watalii
Polisi katika mji wa Mumbai nchini India wametaja maeneo kumi na tano ambayo wametaja kuwa hatari kupiga picha za selfie.
Maeneo hayo ni pamoja na eneo maarufu kwenye ufuo wa bahari la Marine Drive na ufukwe wa Girgaum Chowpatty ambayo yote ni kivutio cha watalii.
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya msichana mmoja mwenye umri wa miaka 18 kuzama baharini akijipiga picha za selfie wiki iliyopita.
Mwaka uliopita, maafisa walipiga marufuku ya picha za selfie katika sherehe za Kihundu kutokana na hofu kwamba huenda kungetokea mkanyagano.
Mabango yaliyosema 'haparuhusiwi picha za selfie" zinaonekana karibu na maeneo ya sherehe hizo katika jimbo la Maharashtra.
Msemaji wa idara ya polisi katika mji wa Mumbai Dhananjay Kulkarni ameiambia BBC kwamba maeneo hayo ambayo ni hatari kupiga picha za selfie ni pamoja na Bandra Bandstand, Sion Fort na Worli Fort ambayo ni maarufu kwa watalii.
Onyo hilo ni baada ya wasichana waliokuwa wakipiga picha za selfie karibu na bahari katika eneo la Bandra walianguka ndani ya maji
"Polisi sasa wataingia katika manispaa ya mji huo ili kuzuia ajali katika maeneo kama haya kwa sababu ya watu wanaopiga picha za selfie Manispaa itatuma maafisa wa uokoaji na kuweka mabango ya tahadhari" amesema bwana Kulkarni.
Onyo hilo la polisi linafuatia tukio hilo la siku ya jumamosi ambapo wasichana wawili waliokuwa wakijaribu kupiga picha za selfie karibu na bahari katika eneo la Bandra kuanguka ndani ya maji.
Mmoja wao alikufa maji na mwingine akaolewa na mtu mmoja aliyekuwa karibu. Mwezi September mtalii kutoka Japan alifariki dunia baada ya kuteleza na kuanguka kwenye ngazi wakati akijaribu kupiga picha ya selfie katika mnara wa Taj Mahal huko Agra.

0 comments:

-