Shirika la afya
duniani WHO limetangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Ebola nchini Liberia
na kusema kuwa maambukizi yote ya ugonjwa huo yamemaliziwa katika eneo
la Afrika Magharibi.
Lakini WHO inasema kuwa bado kazi
haijamalizika. Visa zaidi vinaweza vikaripotiwa na ufuatiliaji wa hali
ya juu utahitajika kuwepo miezi inayokuja.Liberia ilitangazwa kwanza kuwa isiyo na ugonjwa wa Ebola mwezi Mei mwaka 2015 lakini ugonjwa huo ukalipuka tena mara mbili ambapo kisa cha mwisho kiliripotiwa mwezi Novemba mwaka 2015.
Tangazo la leo linatolewa baada ya siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho kutopatikana na virusi vya ebola.
Liberia inajiunga na Guinea pamoja na Sierra Leone ambazo zilipata kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo mwaka uliopita.
Licha ya hilo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ameonya kuwa eneo la Afrika Magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa huo. Ebola umewaua zaidi ya watu 11,000 tangu mwezi Disemba mwaka 2013 .
0 comments:
Post a Comment