Rais Kenyatta ameahidi kuwaandama walioshambulia kambi ya el-Adde
Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta anawatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa
al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa
iliyopita.
Rais Kenyatta atatembelea majeruhi hospitali ya Forces
Memorial, Nairobi na baadaye kujumuika na jamaa, marafiki na maafisa
wakuu wa jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa.Kundi la al-Shabab awali lilisema liliwaua wanajeshi zaidi ya 60 wa Kenya.
Mamia ya jamaa na marafiki wamekuwa wakifika katika vituo vilivyotengwa na idara ya jeshi nchini Kenya kutafuta habari kuhusu wapendwa wao.
Mkuu wa jeshi Jenerali Samson Mwathethe aliambia wanahabari Alhamisi kwamba jeshi bado linaendelea kukusanya habari kuhusu wanajeshi waliokuwa kwenye kambi hiyo.
Alisema bomu lililotumiwa na washambuliaji hao kuvamia kambi hiyo lilikuwa na nguvu mara tatu kushinda bomu lililotumiwa kushambulia ubalozi wa Marekani jijini Nairobi mwaka 1998.
Watu takriban 250 waliuawa kwenye shambulio hilo.
0 comments:
Post a Comment