Katibu
Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (kushoto) akiongea na Waandishi
wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu
Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi
iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya
Stanbink Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bwana
Assah Mwambene.
*********
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, leo amezungumza na waandishi wa
habari Ikulu jijini Dar es salaam kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa
benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa
riba ya mkopo dola Milioni 600 (sawa na Trioni 1.2 za kitanzania) iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.
Amesema kuwa Benki kuu ilipofanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma.
Amesema kuwa Benki kuu ilipofanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma.
Sefue
ameeleza kuwa malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na
baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walishindwa kuvumilia, hivyo tetesi
hizo zikavuja.
Amesema
baada ya tetesi kuvuja, wakaguzi wa benki kuu walifuatilia malalamiko
hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya
mambo ambayo ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki, ambapo fedha
kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa kwenye kampuni ya Kampuni ya Egma
na siku chache zilitolewa zote kwa fedha taslimu wala benki haikukusanya
kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa.
0 comments:
Post a Comment