Kama uliipata stori ya Mamlaka ya Mapato TRA
kunasa makontena tisa eneo la Tanki Bovu Mbezi Dar es Salaam, nina
muendelezo wake mtu wangu kuhusu majibu ya TRA walivyonasa mzigo huo.
Hapa ni nukuu ya alichokisema Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya Walipa Kodi wa TRA >>> ‘Tulipata
taarifa kutoka kwa watu kwamba kuna kontena zinahamishwa kutoka bandari
kavu ya Vingunguti usiku wa manane kuja kwenye godown iliyopo eneo la
Mbezi Tanki Bovu ambayo sio rasmi na haiko kwenye orodha ya bandari kavu
zilizo kwenye uangalizi wa TRA‘>>- Mkurugenzi Richard Kayombo.
Kwenye sentensi nyingine za Richard Kayombo >>> ‘Tumeshirikiana
na Jeshi la Polisi kuhakikisha tunafika eneo hili na kuliweka chini ya
ulinzi…. Hapa yapo makontena tisa, vilevile tumekuta magari matatu
ambayo yalikuwa yanabeba haya makontena, madereva wake wako chini ya
ulinzi.’
Baada ya hapo kilichofatia ni hiki >>> ‘Uchunguzi
wetu tumemfahamu mwagizaji wa makontena pamoja na wakala wa forodha
ambaye alikuwa anashughulikia makontena haya… Makontena yalipata kibali
cha kupelekwa eneo la EPZ Ubungo September 17 2015,
lakini kibali kimepita muda wake na cha kushangaza ni kwamba kontena
hizi zimeletwa huku ambako sio mahali rasmi, ni kiashiria kwamba kuna
jambo baya lilitaka kutokea kama ukwepaji wa kodi.’
Sentensi za mwisho kwenye ufafanuzi huo hizi hapa >>> ‘Tutabaini
kila kitu baada ya kupata nyaraka halisi na kuwapata mwagizaji na
wakala wa forodha ambao wanatakiwa kujitokeza ndani ya saa 24…
wasipojitokea tutafungua makontena kuangalia kilichomo, kama ni bidhaa
halali tutazitaifisha, na kama ni bidhaa haramu zitateketezwa…‘ >>- Richard Kayombo.
0 comments:
Post a Comment