Wednesday, November 4

Denzel Washington.
KATIKA maisha, kila mmoja ana ndoto za kufanikiwa katika maisha. Hata hivyo, wapo watu ambao wamepitia njia ngumu kwenda kwenye mafanikio zilizowafanya kunyanyasika, kudharaulika na hata kupigwa. Wafuatao ni baadhi ya mastaa ambao awali, walionekana si chochote, lakini leo hawakamatiki.

Jennifer Aniston.
Sandra Bullock
HAPANA shaka kwamba Sandra Bullock ni kivutio kwa mashabiki wengi wa filamu na kila mmoja angependa kumuona, achilia mbali kuwa licha ya umri wake wa miaka 50, anaonekana kama kijana kwa miaka kumi nyuma.


icha ya kuwa ni mmoja kati ya mastaa wakubwa kabisa duniani, kazi yake ya kwanza ilikuwa miaka ya 80, alipopata nafasi ndogo ya kuigiza katika filamu ya mauaji iliyoitwa Hangmen. Katika mchezo huo, alitekwa nyara na maofisa wa serikali.
Denzel Washington 
NI jina kubwa miongoni mwa mastaa wa Hollywood, lakini unakumbuka alivyokuja? Mwaka 1974 ilitengenezwa filamu iliyoitwa Death Wish ambayo Charles Bronson alikuwa stelingi wake. Familia moja ilivamiwa na wahalifu huku mkewe akibakwa kabla ya kuuawa.
Baada ya kuvamiwa, familia hiyo ililia sana kuomba wasamehewe, lakini Bronson bila kujali aliwapiga risasi wote wawili. Wa kwanza kupigwa risasi alikuwa ni kijana Denzel Washington, ambaye hata sehemu aliyoigiza haikupewa uzito wowote.

Sylvester Stallone ‘Rambo’.
Sylvester Stallone ‘Rambo’
KATI ya watu ambao majina yao ni alama ya mafanikio ya filamu katika Hollywood, Sylvester Stallone ni miongoni mwao. Alipocheza filamu yake ya kwanza, The Party at Kitty and Stud’s, hakuna mtu aliyedhani staa mkubwa wa baadaye ameanza kutembea. Kuna uvumi kuwa Stallone alilipwa dola 200 tu, filamu ambayo wala haikuonekana nzuri kivile, lakini kwa miaka ile ya 70, kiwango kile ni kama dola 1200 kwa sasa, kiwango ambacho ni kikubwa kwa kazi ya siku mbili!

Nicolas Cage
IWE unampenda au unamchukia, anabaki kuwa Nicolas Cage. Roger Ebert alimhusudu na kumwita muigizaji asiyehofia kuhatarisha maisha yake kwa kucheza sehemu za hatari. Lakini mkali huyu alianzia kung’ara kwenye tamthiliya ndogo miaka ya 80 iliyoitwa Fast Times at Ridgemont High. Hakuna mtu aliyemdhania, lakini kama ukiitazama tamthiliya hiyo leo, utakutana na sura kadhaa zinazo-shine leo katika Hollywood.

Jennifer Aniston
KABLA hajawa kuwa rafiki wa kila mtu na mmoja kati ya waigizaji wa kike wenye majina makubwa katika Hollywood, Aniston alikuwa binti mdogo aliyejaribu kuwa muigizaji huko Tinseltown. Filamu yake ya kwanza ni mwaka 1993, ikiitwa Leprechaun! Ilipotoka ilitakiwa iwe ni komedi, lakini bahati mbaya, ikadharauliwa ile mbaya!

0 comments:

-