Saturday, November 7

STAA asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewacharukia watu wanaohoji kwa nini anapendeza angali mwanafunzi kwa kuwaambia, ‘kwani akiwa mwanafunzi ni mwiko kupendeza?’
Staa asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Lulu alisema amekuwa akiona maon
i ya watu wengi mtandaoni wakihoji anapata wapi fedha za kupendeza wakati yeye ni mwanafunzi hoja ambayo ameiona haina mashiko kwani yeye hatumii fedha nyingi katika urembo wake.
“Watu bwana! Ningekuwa niko rafu wangesema pia na hata hivi ninavyopendeza watu wanachonga pia sasa jamani kipi kitu kizuri ili watu wafurahi na nafsi zao? Mimi umaridadi hapa ndiyo kwake na sijaanza leo, japo sina fedha lakini kidogo nilichonacho kinaficha umasikini,” alisema Lulu.

0 comments:

-