Tuesday, November 10

Kwenye countdown zenye headlines za Siasa, bado macho na masikio ya wengi yako kwenye maeneo machache sasahivi, nani ni Waziri Mkuu TZ? Nani Spika wa Bunge TZ?
Majibu yatapatikana soon ila kwa sasa bado… inawezekana Waziri Mkuu akateuliwa toka chama cha upinzani?
tulia ackson
Dk.Tulia Ackson
Nimempata kwenye exclusive Dk.Tulia Ackson ambaye ni Wakili wa Serikali, ana majibu haya kuhusu uwezekano wa Serikali ya Tanzania kuongozwa na
Waziri Mkuu ambaye anatoka Chama cha Upinzani >>> ‘Sheria inamwezesha kufanya hivyo lakini Katiba imeweka Masharti kwamba Waziri Mkuu atoke wapi, hayo masharti yako matatu.
  1. Ni lazima Waziri Mkuu atoke katika Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Majimboni.
  2. Ni lazima atoke chama chenye Wabunge wengi Bungeni, maana yake ni kwamba Rais akimteua Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi ni lazima ataungwa mkono… lazima Waziri Mkuu aungwe mkono na Wabunge wengi.
  3. Ikitokea hakuna chama chenye Wabunge wengi Bungeni, Rais anaruhusiwa kuteua mtu yoyote ambaye ni Mbunge toka Bungeni.. awe ni Mbunge anayeungwa mkono na Wabunge wengi‘ >>> Dk.Tulia Ackson

0 comments:

-